Ibara ya 18 ya Katiba yetu ya sasa imewekwa kimtego

Ibara ya 18 ya Katiba yetu ya sasa imewekwa kimtego

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Kuelekea mchakato wa Katiba Mpya ni vyema tukaanza kuangazia baadhi ya maeneo yenye ukakasi ndani ya Katiba ya sasa.

Ibara ya 18(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

mwanzo wa kifungu kumewekwa mtego kwa minajili ya kudhibiti uhuru wa maoni.
Serikali imeruhusiwa kutunga sheria ambazo hata kama ni kandamizi zinazokinzana na uhuru wa maoni zinaweza kutumika kudhibiti uhuru huu unaotolewa na Katiba.

Hapo kwenye red paondoke maneno yasomeke:- kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa

mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
 
"There is freedom of speech in Uganda, but I cannot guarantee you freedom after the speech." - Idd Amin Dada.
 
Back
Top Bottom