Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lazaro kwenye hiyo Ibara ya Katiba ni wapi wametumia neno "kushauri" serikali. Mahakama haina kazi ya kushauri.
Sina uhakika hii inakwendaje lakini miezi miwili au mitatu nimesikia BBC kuwa serikali kupitia kwa AG wamekata rufaa, utashindwa kuelewa serikali inalinda maslahi ya nani hapa.
Kwa ninavyoelewa mimi, and that is just the basics, ni kwamba mahakama ndiyo ina wajibu na uwezo wa ku interpret laws, na moja kati ya kazi hizo ni ku ascertain the constitutionality of the said laws./QUOTE]
You are right Pundit.
Huko Mahakamani kuna Mahakimu/Judges. Wao pia sometimes "Wanamisinterpret laws" na kutoa wrong directions/decisions. Thats why kuna APPEALS ambayo ina uwezo wa ku-quash ama kumaintain decision kwa kutokana na facts za kesi husika na ushahidi wa pande mbili (Prosecution/defence).
Ni appeal court pekee ndiyo yenye uamuzi wa mwisho wa kusitisha sheria itayolalamikiwa. Kwa huku chini, of course wanaweza kuona sheria hiyo haipo sahihi na wakaisitisha, it will only work endapo hakutakuwa na rufani. Please correct me if I am wrong.
Lizy
...Mahakama Kuu inapochukua the other option ya kutangaza moja kwa moja kuwa sheria au hatua fulani ni unconstitutional, sheria au hatua hiyo inakuwa unconstitutional mara moja!
Mkjj,
Ref: Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi
ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua
hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili
ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha
hitilafu iliyopo"
Unaelewaje neno Kuamua kutoa fursa?
Lazaros alikuwa anaelezea, na ndio maama neno kuishauri alilifungua na kulifunga. Ref: Lazaros comment, "Mahakama Kuu itachukua option ya "kuishauri" Serikali irekebishe sheria au hatua inayolalamikiwa."
Lizy
Hukumu hiyo ilishatanguliwa na mahakamani ya rufani, ndio maana haijatekelezwa kwa maana hiyo death penalty is still a good law.Nadhani ulikuwa unarejea kesi ya Mbushuu Dominic Mnyaroje vs. RKuna hukumu vilevile ya Jaji Mwalusanya kuwa hukumu ya kifo siyo halali.
Hukumu hii haijatekelezwa hadi leo.
Hapo maana yake mahakama ina discretion,yaani inao uwezo wa ama kuifuta sheria hiyo moja kwa moja toka kwenye vitabu vya sheria kwa kutamka kuwa "this law is unconstitutional and it should be struck out of statute book,and we hereby so do" au ikasema ikasema kwamba sheria hii ni unconstitutional na kutoa mwanya kwa serikali kuirekebisha.
Lizy... hapa itakuwa kazi kidogo.. itabidi ufanye sehemu ya homework hii wewe mwenyewe. Kwa kifupi ni kuwa kulifanyika mabadiliko ya Katiba ambayo yaliingiza kipengele kinachotaka wagombea wa nafasi za uongozi kuwa wanatoka vyama vya kisiasa. Kabla ya hapo mgombea hakulazimishwa kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa. Vipengele hivyo vya Katiba unaweza kuvisoma kwenye Katiba nenda http://www.tanzania.go.tz na utaiona Katiba na uvifuatilie.
Mabadiliko hayo ya vipengele vya Katiba yakapingana na kile kinachoitwa Haki za Msingi (Bill of Rights) ambapo mtu anayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa akitimiza masharti fulani. Itafute hukumu nzima (google Mtikila Vs. Attorney General, Private Candidate"..
Nafurahia reasoning yako M'kijiji. Lakini brother, tutambue tofauti kati ya kesi za jinai na kesi za madai. Utekelezaji wa maamuzi katika kesi hizo vilevile hutofautiana. Hukumu ya kesi ya jinai huanza kutekelezwa mara moja kwa kumwadhibu mkosaji na mkosaji ana haki mbili: kukata rufaa au kuomba bail pending appeal.Kwa upande wa kesi za madai, hukumu ikitolewa, utekelezaji unaanza vilevile mara moja ila aliyeshindwa naye ana haki ya: kukata rufaa na kuiomba mahakama kusitisha utekelezaji hadi rufaa itakaposikilizwa (stay of execution). Ahsante, LazarosJamani, rufaa inapokatwa uamuzi uliotolewa unatiiwa kwanza. Mtu akihukumiwa kufungwa miaka mitano jela, anaenda kwanza lupango wakati kesi yake ya rufaa inasikilizwa. Hatusemi ati kwa vile anakata rufaa basi atoke nje asianze kutumikia kifungo cha awali.
Katika hili, seriikali ilitakiwa kwanza kutii uamuzi wa mahakama wakati inaendelea kukata rufaa, siyo kwamba haitii halafu inakata rufaa, sasa inakata rufaa ya nini wakati status quo is still maintaiened? Wangekata rufaa kama wangekuwa wametii uamuzi wa awali kwanza.
Hii reasoning mnayotumia si ingetumiwa na mamia ya watu ambao tayari wameanza kutumikia kifungo huku wakisubiri rufaa zao? Mfano mzuri ni Aden Rage alipohukumiwa kufungwa si alianza kutumikia kifungo hadi mahakama ya juu ilipotengua hukumu yake?
...Turudi kwenye kesi ya Kikatiba. Ikitokea kesi ambayo hukumu yake inasema "hukumu ya kifo ni kinyume na Katiba kwa sababu inapingana na kipengele kinachosema Kila mtu ana haki ya kulindwa maisha yake n.k" halafu kesho yake kuna hukumu ya mtu kunyongwa je mtu yule anyongwe wakati mahakama inasema sheria inayohalalisha hukumu ya kifo ni kinyume cha Katiba? Tukiangalia ibara ya 30:5 jibu ni ndiyo, kwa sababu ingawa mahakama imesema sheria hiyo ni kinyume na Katiba, sheria hiyo bado ina nguvu na inapaswa kufuatwa.
Tatizo lake ni kuwa hukumu ya Kikatiba haina ulazima wa injunction ya kuizuia serikali nk kutii amri ya mahakama (hata kama ni mahakama ya chini) pending appeal. Kwenye kesi ya kifo, je tukiamua kumuua huyu mtu baada ya hukumu kutolewa na kabla ya rufaa kumalizwa, itakapokuja mwishoni (kwenye mahakama ya rufaa) ikakubaliana na mahakama ya chini kuwa kweli sheria ile ni kinyume na Katiba.. tutawezaje kuhalalisha kitendo hicho cha sisi kama jamii kumuua mtu wakati tumeambiwa na mahakama kuwa ni kinyume na Katiba tangu kabla hatujamuua?
Wakati unasubiri rufaa ya kesi ya Kikatiba maana yale Kesi haijaisha.
Kama Lizy alivyoelezea, Mahakama Kuu inaweza kuwa imekosea. Hawawezi kuanza kuchapisha Vitabu vipya vya Katiba wakati kesi iko katikati ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa!
Mimi tatizo langu sio sana kile kipindi cha giza between the rufaa's and the courts. Tatizo langu ni kile kipindi cha giza wakati tunasubiri Serikali ibadilishe Sheria ambayo Mahakama imeona ni batili lakini imeambiwa na Katiba isithubutu kutamka ni batili.
Kile kipindi pale ndio tatizo langu. Not so much the time between the appeals. Kwa sababu pale kesi haijaisha.
Unanielewa ?
Mimi tatizo langu ni hilo je Mahakama inapotangaza kipengele au sheria fulani ni kinyume na Katiba na serikali inapanga kukata rufaa, je sheria au kipengele hicho kiendelee kutumika? Jibu la kipengele cha 30:5 ni kuwa ndiyo sheriia au kipengele hicho bado kina nguvu na hatuna budi kukitii.
Hakiendelei kutumiaka. Ndio kile kitu kinaitwa stay of execution.
BASIC RIGHTS AND DUTIES ENFORCEMENT ACT, 1994-33, Section 14 (3)
Appeals
Notwithstanding the provisions of the Civil Procedure Code or of any other law to the contrary, where in proceedings under this Act which do not involve continuos breach or personal injuries, the Government files a notice of intention to appeal against any decision of a court the notice shall, when entered, operate as a stay of execution upon the decisions sought to be appealed against.
Sasa hiyo ni kuhusu rufaa. Ambayo mimi sioni tatizo kwa sababu katika ya rufaa na counter-rufaa kesi haijaisha. Yani ule uamuzi wa Mahakama ya Chini sio final. Achana na rufaa. Ukianza kuingiza suala la rufaa hapa unadhoofisha argument na ku obscure uzito wa concern yetu. Kwa sababu kesi bado haijaisha, ndio maana huwezi kusema definitively kwamba sheria ni batili.
Turudi kwenye Ibara ya 30 (5), situation ambapo hakuna rufaa ila tunasubiri Serikali ifute Sheria batili.
Hapo ndio kuna swali. Inakuwaje, kwa mujibu wa ibara ya 30 (5), wakati tunasubiri sheria batili ibadilishwe -uamuzi ambao haujapingwa kwa rufaa - na Serikali inajishaua kubadilisha sheria, kwa nini sheria batili inakuwa bado iko in force?