AL-USTADH
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 406
- 226
Amani iwe nanyi.
Ama baada ya salaam ningependa kuzungumzia mada tajwa hapo juu kama inavyosomeka kuwa ni kwa nini watu hufanya maasi (DHAMBI) wakati anayefanya watu watende dhambi huwa amefungwa kwa muda huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani...?.
IBILIS ni BABA WA MAASI yote unayoyaona yanatokea leo hii duniani, na ushahidi juu ya hili ni pale alipoweza kuwashawishi BABA YETU (ADAM) na MKEWE wakajikuta wakitenda dhambi bila ya wenyewe kujijua na hapo ndipo ilipotokea dhambi ya pili ; dhambi ya kwanza ilitokea pale IBILIS alipomuasi MUNGU WETU na akalaaniwa na akafukuzwa mbinguni na kuahidi atawasimamia WANA WA ADAM kila upande kuhakikisha anaingia nao MOTONI na baada ya hapo ndipo ikafata dhambi ya pili ya kuwashawishi ADAM NA MKEWE kutenda dhambi bila ya kujijua na kusababisha nao pia kufukuzwa mbinguni na kuja duniani ambapo iliandikwa kuwa mwanaume atakula kwa JASHO na mwanamke atazaa kwa UCHUNGU na kujikuta wakiwa MAADUI wenyewe kwa wenyewe kutokana na dhambi zao walizozitenda.
Kizazi baada ya kizazi ikawa vinatenda dhambi juu ya dhambi isipokuwa wale ambao wamesimama upande wa MUNGU, hao pekee ndio hukaa kwenye MSTARI japokuwa nao pia hujikuta wakiteleza na kuanguka kwenye MATOPE ila hunyanyuka haraka na kujisafisha tofauti na wengine ambao huanguka kwenye MATOPE na kuendelea kukaa hapo hapo huku wakiendelea kuyachezea MATOPE pasina kujali.
IBILIS NA SHETANI.
Kama nilivyokwisha sema kuwa IBILIS NI BABA WA MAASI ambaye alikuwa mwenyewe hapo mwanzo lakini baada ya hapo akapata wafuasi, akaendelea kupata kundi na jeshi la kutosha la kufanya kazi moja tu ambayo wala hakuificha aliiweka wazi kabisa kuwa ni kuwakusanya WENZA wa kuingia nao kwenye MOTO WA MILELE na kazi hii hufanywa na MASHEITWAAN wa KIBINADAM na MAJINI ikiwa lengo lao ni hili ; moja tu la kuingia nao MOTONI.
Mashetani wapo wa aina mbili wapo katika MAJINI NA WATU, nikimaanisha kuwa majini na watu wote wameumbwa kwa lengo la kumuabudu MUUMBA WETU sasa wote hawa (MAJINI NA WATU) wanapoasi na kuacha LENGO KUU ambalo ni kumuabudu MUNGU na kufanya mambo ya kumchukiza MUNGU KUPINDUKIA ndipo huingia kwenye sifa hii ya USHEITWAAN ambapo kazi yao KUU inakuwa ni KUMUASI MUNGU na kushawishi wengine pia kufanya MAASI na kumuasi MUNGU.
IBILIS ni kama RAIS ambaye ana jeshi lake sasa RAIS anaposafiri si kwamba eti na jeshi lake linaondoka HAPANA jeshi linabaki na kazi huwa zinaendelea kama kawaida na ndio maana unaweza kuona japo IBILIS amefungwa ndani ya MWEZI MTUKUFU lakini unaweza kujiuliza, kama IBILIS amefungwa mbona bado watu wanatenda dhambi ?, jeshi limebaki katika MAJINI NA WATU, hivyo kama ni mmoja kati ya wenye kufanya MAASI KUPINDUKIA basi juwa kuwa nawe ni mmoja kati ya WANAJESHI na WAFUASI WA IBILIS ambapo japo KIONGOZI hayupo lakini kazi za mikono yake zinaendelea kufanywa kama kawaida.
NAFSI YA MTU NA USHETANI.
Kila nafsi ndani yake imeumbiwa SHETANI ambaye humuamrisha kufanya MAASI na ndio maana mtu anapofanya MAASI utasikia akiambiwa "ISHINDE NAFSI YAKO BWANA" nadhani mmeshasikia hii kauli, na hii ni kwa sababu nafsi yoyote ile imeumbiwa SHETANI ndani yake kwa hiyo tunatakiwa kwanza kupambana na nafsi kwa sababu NAFSI ni kama MTOTO MCHANGA ukiiachia nayo inaendelea tu kutenda MAOVU siku zote ila ukiikataza nayo huacha ni kama MTOTO MCHANGA ukimuachia aendelee KUNYONYA bila ya kumkataza/kumuachisha basi ataendelea KUNYONYA hata awe na umri gani nafsi nayo ni hivyo hivyo kwa sababu nafsi imeumbiwa SHETANI ndani yake.
Sasa hata IBILIS anapofungwa, hapa mtu huwa anashindwa na nafsi yake na kushindwa kuikataza na kuizuia katika kufanya MAASI sasa ukiona upo kwenye hali hii au kundi hili basi juwa wazi kuwa nawe ni mmoja kati ya waliopo chini ya UTAWALA wa IBILIS japo RAIS hayupo lakini kazi za mikono yake huendelea kufanyika pasina kipingamizi na wala sio kazi za mikono yake huendelea kufanyika pasina kipingamizi na wala sio kipindi cha kumsingizia IBILIS eti ndio anakushawishi LA HASHA hapa ni wewe na nafsi yako na wala sio IBILIS kwa sababu ndani ya MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAAN IBILIS hufungwa MINYORORO na MALAAIKA WA MUNGU na ndio maana unapoisha mwezi huu basi IBILIS huwa anaachiliwa na huwa anarudi kwa HASIRA mno na ndio maana utaona watu wakitenda MAASI/MAOVU kwa kasi mno tofauti na alivyokuwa amefungwa hapo kabla.
Ukiona upo kwenye MAASI ndani ya MWEZI HUU basi juwa wazi kuwa MOYO WAKO umeota KUTU na umezidiwa na IBILIS kwa kupigwa MUHURI NA IBILIS na ndio maana unaona MKUU hayupo lakini MTUMISHI unatumikia kama kawaida na kuendelea kufanya kazi za MKUU hata kama yeye hayupo............kwa mfano wa haraka haraka chukulia tu kama vile unaendesha BAISKELI kisha ukanyonga itategemea ulikuwa unanyonga kwa kiasi gani, utaweza kuona hata kama utaacha kunyonga pedeli lakini BAISKELI utakuta inaendelea tu kutembea katika spidi ambayo ulikuwa unainyongea itategemea ulikuwa ukinyonga kwa spidi kiasi gani BAISKELI hiyo.Hii ni sawa na mfano wa IBILIS kuwa, hata kama AMEFUNGWA inategemea ulikuwa ni MFUASI WAKE kwa kiasi gani na ndio maana unakuta hata kama YEYE HAYUPO lakini MTUMISHI unaendelea kutumikia kwa kutenda MAASI/MADHAMBI kama kawaida pasina kujali uwepo wa MKUU AU LAA.
Hivyo, kwa kuweza kujua tatizo ni KWA NINI WATU HUTENDA MADHAMBI WAKATI MSHAWISHI KAFUNGWA tunaweza kujua kuwa kumbe ni NAFSI ZETU wenyewe na wala sio sababu ni IBILIS, hivyo kaa chini utafakari na ujaribu kuizuia nafsi yako kama unavyomzuia MTOTO MCHANGA KUNYONYA, kama utamuachia aendelee KUNYONYA basi ataendelea tu pasina kuacha mpaka pale utakapo muachisha mwenyewe au aidha kama utaizuia na kuweza kupambana na kuishinda nafsi yako basi MUNGU nae atakuonyesha NJIA kwa sababu alishasema MUNGU kuwa, anamuongoza MTU kule MTU anapotaka mwenyewe kwenda kama ukitaka kwenda KULIA basi MUNGU atakufanyia wepesi na atakuongoza katika NJIA HIYO unayotaka kwenda, na pia ukitaka kwenda KUSHOTO pia atakufanyia wepesi na atakuongoza pia katika NJIA HIYO unayotaka kwenda.
Nawatakia kila la heri.