Ibn Khaldun (1332-1406) na kodi

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Huyu jamaa alizaliwa mwaka 1332 huko Mji wa Tunis leo. Alikuwa msomi wa Quran na sheria za kiislamu. Pia alikuwa Afisa wa serikali.
Ni moja ya wanafalsafa wanaoheshimika sana. Alizungumza mambo mazuri sana kuhusu kodi, alisema kuwa..

Serikali inapoanza kodi huwa ni kwaajili ya kufanyia mambo muhimu kwa ajili ya wananchi na kwaajili ya kuendesha serikali. Kadri inavyoendelea na kustaarabika ndipo viongozi huzidi kuongeza kodi ili kugharamia maisha yao ya anasa.

Anasema hii ni kuwakosea haki wananchi na pia kunarudisha nyuma maendeleo sababu kodi kubwa husababisha uzalishaji mali kupungua

Na uzalishaji ukipungua baada ya muda na kodi nayo hupungua. Kwahiyo kodi kubwa hufanya baadaye kodi isipatikane. Hili wazo lilikuja kufufuliwa na mwanauchumi wa Marekani Arthur Laffer mwaka 1974.

Historia na vitabu ina mengi ya kutufunza ili tusirudie makosa ya zamani.

cc Malcom Lumumba , Wick , zitto junior
 
Ila mkuu Giant hivi kuja serikali inaweza kujiendesha bila kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiwezekani ila kunatakiwa kuwr na balance ili production isisimame. Watu leo hawataki kulima kahawa na chai sababu kodi zinachukua sehemu kubwa ya mapato yao.
huyu mchumi wa kimarekani ndiyo alifanya kazi ya kutafuta balance ilipo.
 
ndo maana JIWE kaamua kupunguza kodi kwenye bia?
 
Huyo ndiye Abdulrahman Mohammed ibn Khaldun.
Kitabu chake kinaitwa Muqqadimah likitab alibar
 
Umenikumbusha mbali na huyu Ibn Khaldum
 
Ibd khaldun ni miongoni mwa mediaval philosophers wakujivunia sana katika Afrika yetu hasa ktk kutengeneza balance katika jamii zetu ingawa wanafalsafa wengi wa kizungu wanampinga kwasababu za kidini ila mafundisho yake ni mfano wa kuigwa ktk jamii zetu za sasa
 
Kati ya hayo mengi aliyo ya sema na kuyafanya isisahau huyu Mohamed Akhemed ibn khaldun no mwanafalsafa na reformer Mkubwa wa Imani ya kiislam,cha kufurahisha reformers wa imani kubwa duniani wametoka Afrika akiwepo reformer wa Dini ya katoliki Sent Augustine Bishop of Hippo raia wa Algeria.Afrika tuna mchango Mkubwa sana katka imani za wenzetu,sjui kwann tumeahindwa kuzfanyia Reformation dinizetu za fasili kuwa imani moja kama wenzetu: Hindu(India),Buddha(india),confusion(china),Taoism(china),lslam(warabu),christian(wazungu),Judaism(jiwish),AFRIKA---- .Why not Afrika.
 
Kweli Afrika ilikuwa imepiga hatua muda mrefu sana, maandiko ya huyu jamaa yametumiwa na wanazuoni wengi tuu juu ya mifumo yakinifu ya kodi katika mataifa yao japo wengi wameshindwa kumpa credit, sijui kwa kuwa alitoka Afrika!
 
Naskia huyu jamaa alikuwa ni genious sana,kuna mdau wangu mmoja pale mwalim nyerere ni lecturer wa mambo ya historia aliwahi kusema kuwa huyu jamaa shida yake alikuwa haandiki mambo mengi sana,ikamfanya idea zake nyingi zisifahamike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…