Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Huyu jamaa alizaliwa mwaka 1332 huko Mji wa Tunis leo. Alikuwa msomi wa Quran na sheria za kiislamu. Pia alikuwa Afisa wa serikali.
Ni moja ya wanafalsafa wanaoheshimika sana. Alizungumza mambo mazuri sana kuhusu kodi, alisema kuwa..
Serikali inapoanza kodi huwa ni kwaajili ya kufanyia mambo muhimu kwa ajili ya wananchi na kwaajili ya kuendesha serikali. Kadri inavyoendelea na kustaarabika ndipo viongozi huzidi kuongeza kodi ili kugharamia maisha yao ya anasa.
Anasema hii ni kuwakosea haki wananchi na pia kunarudisha nyuma maendeleo sababu kodi kubwa husababisha uzalishaji mali kupungua
Na uzalishaji ukipungua baada ya muda na kodi nayo hupungua. Kwahiyo kodi kubwa hufanya baadaye kodi isipatikane. Hili wazo lilikuja kufufuliwa na mwanauchumi wa Marekani Arthur Laffer mwaka 1974.
Historia na vitabu ina mengi ya kutufunza ili tusirudie makosa ya zamani.
cc Malcom Lumumba , Wick , zitto junior