Ibra Da Hustler ndani ya Sober House!

Ibra Da Hustler ndani ya Sober House!

Wamtaa huu

Senior Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
168
Reaction score
55
Msanii wa hiphop Ibra Da Hustler amepelekwa rehab ndani ya Kigamboni Sober House!

Akiongea kwa simu kupitia kipindi cha XXL cha clouds fm mama mzazi wa msanii huyo amesema amelazimika kumpeleka huko mtoto wake kwa kuwa hali yake ya hivi karibuni imekuwa mbaya zaidi.Amekuwa ni mtu wa kuhitaji sana fedha kwake ili akatumie madawa hayo ya kulevya.Mama huyo aliweka wazi kuwa siku za nyuma waliwahi kujadiliana kuhusu kwenda huko sober house na Ibra alikubali lakini akawa anapiga chenga.

"Juzi aliniomba laki mbili anataka kusafiri kwenda Bukoba.Nilimwambia sina hela kwa kuwa nilijua kuwa atazidi kujiumiza na madawa.Alikasirika sana akasema kama hapati hiyo hela basi atachukua jiko au laptop akauze ili apate kusafiri.Na akasisitiza kama sio hivyo basi nimpe mtu laptop atoe laki 2 ili nikipata nimrudishie".Aliendelea kusema mama Ibra.

Baada ya kuona hali hiyo ndipo mama alipoamua kuwasiliana na watu wa sober House na wakaja wakafanikiwa kuondoka na Da hustler.Hiyo ni baada ya mama kumdanganya kijana wake kuwa aende nao hao watu wakampe hiyo laki mbili.

Ibra Da Hustler ni mwanahiphop aliyewahi kuwa kundi la nako2nako na anasikika kwenye nyimbo kama "Ndio zetu" na "Hawatuwezi".Baadae alijitoa na baada ya kupishana kimaslahi na wenzake akina Gnako,Bunako na Lord Eyes.Huyu Lord Eyes naye ndiye yule ambaye hupatwa na mikasa inayosadikiwa ni kwa sababu ya matumizi ya mihadarati.Aliwahi kushutumiwa kuiba vifaa vya gari la msanii "mbana pua" Ommy Dimpoz.Pia wiki iliyopita huyo Lord ameshutumiwa kuiba vifaa vya gari la mdada mmoja jijini Arusha.

Hali hiyo imesababisha asimamishwe kwenye kundi la Weusi linaloundwa na wanahiphop kadhaa wanaotoka Arusha.

Habari ndo hiyo.Swali ni je hiphop bila madawa haiwezekani?
 
Madawa gani unamaanisha mkuu kwa sababu bangi siyo madawa ya kulevya , bangi ni mmea kama ilivyo mchicha,nk ila kama jamaa anakula poda he should stop it now ila kama bangi muache ale mmea.
 
Nilipata bahati ya kusikiliza wakati mama yake anaongelea hilo swala,jamaa alifikia hatua mbaya sana,hakuna mwanamke zaidi ya mama aisee amefanya kadri alivyoweza kuhakikisha Ibra anapelekwa Sober
 
Kuna kijana ana tatizo kama hili itabidi niwatafute hawa jamaa wa Kigamboni watusaidie aisee.Madawa yanatuharibia nguvu kazi kwa kasi ya kutisha.
 
Watayasingizia mno hayo madawa mbona sie hatuna mpango nayo wao wanayapendea ninii?
 
Kauli yako iko deep sana. Hasa kwa sababu haina chembe ya "political correctness" inayoweza kuanza ku equivocate mambo kwa habari nyingi ambazo ni za kutuchuuza tu tuamini kwamba habari ya madawa ni ugonjwa.

Ulimwengu wa ustaarabu na "political correctness" sasa hivi umeshapitisha kwamba uteja wa madawa ni kama ugonjwa, na hivyo hawa watu wanatakiwa kuangaliwa kama wagonjwa wasiojiweza.

Amefariki actor mmoja hivi karibuni New York City, kwa hwroin overdose, watu badala ya kulaani utumiaji wa madawa wamemsifu alivyokuwa actor mzuri na kumhurumia kwa "ugonjwa wake".

Madogo wanaangalia wanaona kumbe haya mambo poa tu, unajidunga mpaka unakufa, halafu watu wanakushobokea vilevile.

Lakini wote tunajua kwamba, hata kama leo hawajiwezi kwa uteja, kuna wakati waliamua kuanza kwa makusudi.
 
Mbona alisema ameacha kula ngada.NAKO 2 NAKO NDO IMEKWISHA TAYARI.
 
Afadhalii umeandikaa lugha yetu maaana ungenishushiaa ma ung'eng'e ingekua balaaa!!
 
Kundi zima la N2N wote wanakula unga

Sidhani kama GNako anakula unga,nakumbuka enzi hizo wako on fire (2006-2009) Kwenye kundi lao GNako ndio alikuwa anaonekana Brazameni Lord Eyez,Bou Nako na Ibra hawa walikuwa wanavuta bangi
 
Ninja after Ninja wanafeli daily noma sana Mungu amrudishie afya yake,yeap Bou Nako ni drugs free yule jamaa ni ngumu kuamini hata mmea hapandishi jamaa yuko clean mby.
 
Madawa gani unamaanisha mkuu kwa sababu bangi siyo madawa ya kulevya , bangi ni mmea kama ilivyo mchicha,nk ila kama jamaa anakula poda he should stop it now ila kama bangi muache ale mmea.
Acha upotoshaji hakuna aliyeanza kula poda bila ya kwanza kula huo unaouita mmea,unakula bangi inafika muda stimu zake unaona za kawaida tu so unarukia huko kwenye poda ukiamin utapata stimu za juu kabisa,utatoa mifano mingi sana but jua mvuta bangi ana hatar kubwa ya kuvuta unga,so usifanye kampen zisizo na maana kuhusu huo mjan wako
 
Kutumia madawa ya kulevya sio kwamba ni ulemavu uliozaliwa nao au ugonjwa! we kama unatumia tumia tu.na janga ni lako na sio la kitaifa kama inavyo elezwa!.
 
Sidhani kama GNako anakula unga,nakumbuka enzi hizo wako on fire (2006-2009) Kwenye kundi lao GNako ndio alikuwa anaonekana Brazameni Lord Eyez,Bou Nako na Ibra hawa walikuwa wanavuta bangi

Ukiwa blazameni unga hauwezi kula au?
 
Ukiwa blazameni unga hauwezi kula au?

Wakati huo(2005-2009) ilikuwa ngumu sana kuamini Gnako anaweza kuwa kundi moja na hao jamaa, Lord Eyes Ibra na Bou Nako walikuwa wanaendana but GNako alikuwa tofauti.Jamaa walivyohamia Dar ndio Lord na Ibra walianza kupotea
 
Msanii wa hiphop Ibra Da Hustler amepelekwa rehab ndani ya Kigamboni Sober House!

Akiongea kwa simu kupitia kipindi cha XXL cha clouds fm mama mzazi wa msanii huyo amesema amelazimika kumpeleka huko mtoto wake kwa kuwa hali yake ya hivi karibuni imekuwa mbaya zaidi.Amekuwa ni mtu wa kuhitaji sana fedha kwake ili akatumie madawa hayo ya kulevya.Mama huyo aliweka wazi kuwa siku za nyuma waliwahi kujadiliana kuhusu kwenda huko sober house na Ibra alikubali lakini akawa anapiga chenga.

"Juzi aliniomba laki mbili anataka kusafiri kwenda Bukoba.Nilimwambia sina hela kwa kuwa nilijua kuwa atazidi kujiumiza na madawa.Alikasirika sana akasema kama hapati hiyo hela basi atachukua jiko au laptop akauze ili apate kusafiri.Na akasisitiza kama sio hivyo basi nimpe mtu laptop atoe laki 2 ili nikipata nimrudishie".Aliendelea kusema mama Ibra.

Baada ya kuona hali hiyo ndipo mama alipoamua kuwasiliana na watu wa sober House na wakaja wakafanikiwa kuondoka na Da hustler.Hiyo ni baada ya mama kumdanganya kijana wake kuwa aende nao hao watu wakampe hiyo laki mbili.

Ibra Da Hustler ni mwanahiphop aliyewahi kuwa kundi la nako2nako na anasikika kwenye nyimbo kama "Ndio zetu" na "Hawatuwezi".Baadae alijitoa na baada ya kupishana kimaslahi na wenzake akina Gnako,Bunako na Lord Eyes.Huyu Lord Eyes naye ndiye yule ambaye hupatwa na mikasa inayosadikiwa ni kwa sababu ya matumizi ya mihadarati.Aliwahi kushutumiwa kuiba vifaa vya gari la msanii "mbana pua" Ommy Dimpoz.Pia wiki iliyopita huyo Lord ameshutumiwa kuiba vifaa vya gari la mdada mmoja jijini Arusha.

Hali hiyo imesababisha asimamishwe kwenye kundi la Weusi linaloundwa na wanahiphop kadhaa wanaotoka Arusha.

Habari ndo hiyo.Swali ni je hiphop bila madawa haiwezekani?

Lord Eyes Mbaya sana aisee,
Kamuharibu Ray C, Kamuharibu pia na huyu Ibra da Hustler, sijui G-Nako na Bu-Nako wako kwenye hali gani.
 
Hivi hawa jamaa niaje wanakuwa watumiaji badala ya kuwa wauzaji

Wasanii wa hiphop wa USA wamepata utajiri kupitia biashara hiyo sio kwa kutumia
wajifunze maisha ya Biggie na Jay Z
 
Mkuu, Jay Z na Biggie hawajatajirika kwa kuuza unga. Walikuwa street pushers tu waki-hustle kupata hela ya kula. Muziki ndio uliwatoa.
 
Back
Top Bottom