Wamtaa huu
Senior Member
- Jan 21, 2011
- 168
- 55
Msanii wa hiphop Ibra Da Hustler amepelekwa rehab ndani ya Kigamboni Sober House!
Akiongea kwa simu kupitia kipindi cha XXL cha clouds fm mama mzazi wa msanii huyo amesema amelazimika kumpeleka huko mtoto wake kwa kuwa hali yake ya hivi karibuni imekuwa mbaya zaidi.Amekuwa ni mtu wa kuhitaji sana fedha kwake ili akatumie madawa hayo ya kulevya.Mama huyo aliweka wazi kuwa siku za nyuma waliwahi kujadiliana kuhusu kwenda huko sober house na Ibra alikubali lakini akawa anapiga chenga.
"Juzi aliniomba laki mbili anataka kusafiri kwenda Bukoba.Nilimwambia sina hela kwa kuwa nilijua kuwa atazidi kujiumiza na madawa.Alikasirika sana akasema kama hapati hiyo hela basi atachukua jiko au laptop akauze ili apate kusafiri.Na akasisitiza kama sio hivyo basi nimpe mtu laptop atoe laki 2 ili nikipata nimrudishie".Aliendelea kusema mama Ibra.
Baada ya kuona hali hiyo ndipo mama alipoamua kuwasiliana na watu wa sober House na wakaja wakafanikiwa kuondoka na Da hustler.Hiyo ni baada ya mama kumdanganya kijana wake kuwa aende nao hao watu wakampe hiyo laki mbili.
Ibra Da Hustler ni mwanahiphop aliyewahi kuwa kundi la nako2nako na anasikika kwenye nyimbo kama "Ndio zetu" na "Hawatuwezi".Baadae alijitoa na baada ya kupishana kimaslahi na wenzake akina Gnako,Bunako na Lord Eyes.Huyu Lord Eyes naye ndiye yule ambaye hupatwa na mikasa inayosadikiwa ni kwa sababu ya matumizi ya mihadarati.Aliwahi kushutumiwa kuiba vifaa vya gari la msanii "mbana pua" Ommy Dimpoz.Pia wiki iliyopita huyo Lord ameshutumiwa kuiba vifaa vya gari la mdada mmoja jijini Arusha.
Hali hiyo imesababisha asimamishwe kwenye kundi la Weusi linaloundwa na wanahiphop kadhaa wanaotoka Arusha.
Habari ndo hiyo.Swali ni je hiphop bila madawa haiwezekani?