Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu!
Inakuaje kwa waliochangia pesa ya kumlipa Harmonize ili avunje Mkataba wake?
===
Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Ibraah, ambaye alikuwa chini ya lebo ya Konde Gang, sasa ni huru rasmi kuendelea na kazi zake za muziki kama msanii huru. Hii inafuatia makubaliano yaliyofikiwa leo kati yake na uongozi wa lebo hiyo, baada ya mgogoro uliodumu kwa takriban wiki mbili.
Makubaliano hayo yamesainiwa mbele ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana. Katika kikao hicho, Ibraah aliambatana na mshauri wake wa biashara, Bw. Msigwa, huku upande wa lebo ya Konde Gang ukiwakilishwa na wakili wao, Bi. Sandra.
Kupitia makubaliano hayo, Ibraah ameruhusiwa kuendelea na kazi zake za muziki bila masharti yoyote kutoka kwa lebo hiyo. Hatua hii inatoa nafasi kwa msanii huyo kujiendeleza zaidi kisanaa kwa uhuru na ubunifu wake binafsi.
Soma, Pia