Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Msanii Ibraah kutoka Konde Gang ameweka rekodi ya kihistoria baada ya kuweka video ya wimbo wake mpya uitwao "rara".
Wimbo huo umeweka rekodi ya kupata views zaidi ya laki tatu chini ya dakika moja. Rekodi hiyo inasemekana ni ya kwanza kutokea kwa msanii wa Afrika Mashariki na kati.
Mpaka sasa wimbo huo umepunguza kasi ya kupata views na kufikisha views laki sita katika mtandao wa YouTube hali iliyopelekea kuleta minong'ono kuwa msanii huyo amenunua views na kufanya makosa ya kuzifungulia zote kwa wakati mmoja alipoachia video yake.