Wahenga waliwahi kunena..
“Uongo unaoishi ndiyo ukweli mpaka ukanushwe."
Siku mbili zilizopita mwandishi wa habari za michezo nchini Tanzania, Edo Kumwembe aliandika makala katika gazeti la mwanaspoti yenye kichwa cha habari
Ajib ni mwanasoka aliyetoka Masaki?.
Katika makala hiyo Edo anashangaa tena [eeeh tena, kwa kua msimu uliopita aliandika makala yenye maudhui hayo hayo] ni kwanini mpaka sasa "mchezaji bora kwa sasa nchini Tanzania"
Ibrahim Ajibu wa Simba S.C hasongi mbele, yupo pale pale.
Edo ametoa sababu lukuki, za kwanini
Ibrahim Ajibu kagota sehemu, na kwanini hasongi mbele.. Asilimia kubwa ya hizo sababu ni za kusikia sikia..
Mfano, namnukuu..
"Hata hivyo, majuzi nikawasikia baadhi ya watu wa Simba wakidai kwamba, Ajib na baadhi ya wachezaji wa zamani wa Simba wanakerwa na sifa nyingi wanazopewa wachezaji wapya wa Simba ambao wanaonekana kama vile wamekuja kuiondoa Simba katika utumwa wa miaka minne dhidi ya Yanga na Azam.
Nimesikia kwamba wachezaji wa zamani wanaamini kuwa viongozi wa Simba wanawajali zaidi wachezaji wapya. Inadaiwa kuwa hata pasi huwa hawawapi wachezaji wapya."
Hapa haihitaji hata elimu ya chekechea ili uweze kun'gamua kua hao wachezaji wapya ni kina nani.. Wachezaji wapya Simba S.C ambao wanasumbua katika vyombo vya habari ndani na nje ya nchi ni
Mavugo na
Blagnon, naimani ndio anaowazungumzia.
Leo,
Ibrahim Ajibu akihojiwa na
SALEHJEMBE amekanusha vikali hizo habari za kusikia sikia katika vijiwe vya kahawa..
Namnukuu..
"Uwepo wa Mavugo katika kikosi chetu kunanisaidia kuwa na morali ya hali ya juu na kunipa hamasa pindi ninapokuwa naye uwanjani hivyo natarajia kuwa vizuri zaidi msimu huu tofauti na msimu uliopita. Wanasimba watarajie kile ambacho wanakitarajia kukipata, kwani lazima tutatwaa ubingwa."
Neno langu kwa Edo Kumwembe
1. Msimu huu
Ibrahim Ajibu kauanza kwa kasi sana, na naimani ndio msimu wake wa mwisho kucheza Bongo. Na nadhani ni kutokana na kufanyia kazi ushauri uliompatia msimu uliopita katika makala ndeeefu uliyomuandikia, ambayo maudhui yake hayana tofauti na hii ya juzi.
2. Simba ya sasa ni imara tofauti na unavyosikia sikia mitaani au katika vijiwe vya kahawa.
Hiyo migogoro mnayotaka kuianzisha kwa lazima baina ya "wazawa" na "wakuja" kamwe haitatokea. Huu moto tuliouasha hakuna wa kuuzima, ni kugawa dozi tu mpaka msimu unaisha.
SIMBA SPORTS CLUB NGUVU MOJA