Ibrahim Class amtwanga Mzimbabwe

Ibrahim Class amtwanga Mzimbabwe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Bondia wa Tanzania, Ibra Class (Mawe) amemshinda kwa TKO dhidi ya Bondia wa Zimbabwe, Ndodana Ncube.

Pambano hilo lilikuwa la roundi kumi lakini kufikia roundi ya nane Ndodana Ncube kuanguka na kushindwa kuinuka baada ya kuhesabiwa.

Pambano hilo lilifanyika viwanja vya Mkwakwani, Tanga, usiku wa kuamkia Januari 29, 2023.
 
1. Huyu Sasa aende nje ya nchi akapeperushe bendera . Asiwe Kila siku anatumia mazingira ya nyumbani tuu.

2. Waandaaji wa boxing Kuna version ya Wimbo wa Taifa mnaptumia kwenye hizi ndondi siku zote imekuwa haipo sawa. Ina pause ndefu Sana katikati ya Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania na kuwafanya watu waanze kushangilia katikati ya wimbo wakidhani kama umeisha. Hii inasababisha usumbufu. Version zipo nyingi Sana. Wasilianini na Doctor Mapana pale idara ya muziki UDSM au nendeni kwenye kwaya za kikatoliki za MT. Kizito makuburi au ST. John Paul choir pale mbeya. Watawarekodia kitu Bora kabisa hata ukiwa unaimbwa ile sovereignty ya nchi itaonekana
 
Back
Top Bottom