Mbangaizaji wa Taifa
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 493
- 844
Naona mdogo mtu akiwa anamsapoti Freeman Mbowe wakati kaka mtu yeye akiwa anamsapoti Lissu,
Msikilize jamaa kamchana chana vibaya Freeman Mbowe kwa hoja tano.
======================
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Makete, Ibrahim Ngogo, ametoa wito kwa wajumbe wa chama hicho kumpigia kura Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu, katika uchaguzi wa uenyekiti wa taifa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Ngogo amesema kuwa Lissu ametoa mchango mkubwa kwa chama, akitaja kuwa nusu ya maisha yake ameyaweka rehani kwa ajili ya kukitetea CHADEMA na wananchi wa Tanzania.
Ngogo amesisitiza kuwa ni wakati wa Freeman Mbowe kuachia nafasi ya uenyekiti na kumpa fursa Lissu ili kuimarisha chama na kudumisha amani nchini.