Ibrahim Traoré: Sitaki Polisi Watembee na Bunduki Nchini kwangu, Wananchi Hawapaswi kuishi Kwa Uoga Rais Ibrahim Traore

Ibrahim Traoré: Sitaki Polisi Watembee na Bunduki Nchini kwangu, Wananchi Hawapaswi kuishi Kwa Uoga Rais Ibrahim Traore

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,112
Reaction score
34,951
1778090862738.png

Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré, ameendelea kusisitiza umuhimu wa amani na mshikamano kati ya vyombo vya dola na wananchi, kwa kueleza kuwa hataki polisi wake kutumia vitisho kwa raia wala kutembea na bunduki kwa namna inayoweza kuleta hofu kwa wananchi.

Traoré amesema lengo lake ni kuona wananchi wa Burkina Faso wanaishi kwa utulivu, amani na kujiamini bila kuhofia vyombo vya usalama. Amesisitiza kuwa polisi wanapaswa kuwa walinzi wa wananchi na si chanzo cha hofu katika jamii.

Kauli hiyo imeendelea kuvutia mjadala mkubwa ndani na nje ya Afrika, huku wengi wakitafsiri msimamo wake kama sehemu ya juhudi za kujenga uhusiano mzuri kati ya serikali na wananchi wake.
Aidha, Traoré ameweka msisitizo katika ulinzi wa haki za wananchi pamoja na kuhakikisha usalama unazingatia utu, heshima na amani ya jamii.

Kidume hiki Rais Ambae anayefaa kuigwa barani Afrika ndio huyu.
 
Kitu kama hicho hakiwezekani Tanzania ambapo rais anaamini kabisa kwamba bunduki ndio mlinzi wa utawala wake kwani anajua fika namna gani aliingia madarakani.
 
Ni suala muda tu Dogo wanamuua

Ngoja Putin awekwe mezani kwa dau nono tutasikia kila mlio
 
Mkuu kila nikitumia condom nachelewa kumwaga hii itakua shida nini.
411442.jpg
 
Back
Top Bottom