poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 453
- 175
Mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic amekashifu vikali tabia ya wachezaji wa Chelsea ya kumzingira refa katika mechi yao ya muondoano katika ligi ya mabingwa ya Ulaya. Akizungumzia tabia hiyo Zlatana alisema kuwa alihisi kama aliyezungukwa na watoto wadogo 11. Ibrahimovic alihisi kwamba jambo hilo lilimshinikiza refa kutoa kadi nyekundu.
Ingawa PSG walionesha ujasiri na ushupavu mkubwa kwa kuwadhibiti Chelsea wakiwa na wachezaji 10 na kuweza kutoka sare ya 2-2 na kufuzu kwa robo fainali, Ibrahimovic hataruhusiwa kucheza katika michuano hiyo.
Tabia hiyo ya kumzunguka refa imeibua kashifa kubwa kutoka kwa wachezaji, wakufunzi na wataalamu wa kandanda huku Rais wa UEFA Michel Platini akiapa kumaliza tabia hiyo katika michuano ya Ulaya.
Katika mahojiano baada ya mechi hiyo mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho alisema kuwa hakudhania kama Ibrahimovic alipaswa kuonyeshwa kadi nyekundu na kwamba anatumai kuwa UEFA itachukua hatua ya kutupilia mbali uamuzi huo.