Ibrahimovic: Nilihisi kama nimezingirwa na vitoto 11

Ibrahimovic: Nilihisi kama nimezingirwa na vitoto 11

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
453
Reaction score
175
Mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic amekashifu vikali tabia ya wachezaji wa Chelsea ya kumzingira refa katika mechi yao ya muondoano katika ligi ya mabingwa ya Ulaya. Akizungumzia tabia hiyo Zlatana alisema kuwa alihisi kama aliyezungukwa na watoto wadogo 11. Ibrahimovic alihisi kwamba jambo hilo lilimshinikiza refa kutoa kadi nyekundu.
Ingawa PSG walionesha ujasiri na ushupavu mkubwa kwa kuwadhibiti Chelsea wakiwa na wachezaji 10 na kuweza kutoka sare ya 2-2 na kufuzu kwa robo fainali, Ibrahimovic hataruhusiwa kucheza katika michuano hiyo.

Tabia hiyo ya kumzunguka refa imeibua kashifa kubwa kutoka kwa wachezaji, wakufunzi na wataalamu wa kandanda huku Rais wa UEFA Michel Platini akiapa kumaliza tabia hiyo katika michuano ya Ulaya.
Katika mahojiano baada ya mechi hiyo mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho alisema kuwa hakudhania kama Ibrahimovic alipaswa kuonyeshwa kadi nyekundu na kwamba anatumai kuwa UEFA itachukua hatua ya kutupilia mbali uamuzi huo.
 
cha ajabu the want to punish zlatan for more because of that speach
 
safi sana aliongea ukweli sijui sheria za mpira ila sikuona sababu ya zlatan kutolewa nje kwa red card....Chelsea walijua ni advantage kumbe daaah
 
Vitoto 11 vinakaribia kuchukua ubingwa Wa EPL, stay tuned
 
Mbavu zangu umezivunja mkuu
Mkuu Chelsea wana tabia kama za mabinti, ile rafu kama mwamuzi asingesongwa isingetoka kadi nyekundu.
Yule Oscar alivoguswa tuu kajirusha na kulalamika utadhani kaumia sana vile, ila mwisho wa siku haki imesimama upande wake.
 

Attachments

  • 1426276515696.jpg
    1426276515696.jpg
    36.7 KB · Views: 209
Back
Top Bottom