Tetesi: ICC Ndani ya Tanzania

Tetesi: ICC Ndani ya Tanzania

Mwingereza

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
1,115
Reaction score
2,771
Habari nilizozipata muda siyo mrefu ni kwamba, Wachunguzi wa maakama ya kimataifa (International Criminal Court) ya ICC, tayari wamefika Tanzania kwa kazi maalum.

Haifaamiki wako wapi, lakini inasemekana tayari wamefanya maongezi na baadhi ya viongozi wa haki za binadamu Tanzania.

Huu nadhani ni ujumbe fika kwa Makonda, Mwigulu, Jeshi la polisi na bosi wao, "Mungu mtu wa Tanzania " Kuwa makini kwani inawezekana wakaingia the Hague.
 
umeandika kishabiki na kizushi mno
 
Icc wanaangalia mambo mengi sana, kuna wengine wanakuwa ni waroho wa madaraka wanakuwa wanaanzisha migogoro isiyokuwa na sababu ili nchi isitawalike kwa tanzania hilo halitawezekana. Ile mahakama haikanzishwa kwa ajili ya wanaokosea tu bali ni pamoja na wanaoandaa mipango ya vurugu ktk nchi
 
Hivi Najiuliza zile recorded clips za JKN siku hizi zimepigwa marufuku kwenye TV Station zetu?Au wa naogopa Kesi za Uchochezi?
 
Karibuni sanaaa ICC itabidi waanze na Mwigulu na mwenzake Makonda maana hao ndio wanao hii nchi ni yao..Hivi Chadema wakiachiwa wakaandamana nini kitafanyika kibaya hivi kuna siku hata moja chadema wameruhusiwa kuandamana ila.CCM ni ruksaaa kabisaaa...
 
ICC haiwezi kuhusika na kesi ndogo kama za Tanzania.
 
Wamekuja kwa ajili ya ile kesi ya Chadema? Acheni kuwahadaa wanachama wenu, kila siku usanii unaongezeka au yule mtaalam wa sanaa mliyesajili mwaka jana analeta haya?
 
Icc wanaangalia mambo mengi sana, kuna wengine wanakuwa ni waroho wa madaraka wanakuwa wanaanzisha migogoro isiyokuwa na sababu ili nchi isitawalike kwa tanzania hilo halitawezekana. Ile mahakama haikanzishwa kwa ajili ya wanaokosea tu bali ni pamoja na wanaoandaa mipango ya vurugu ktk nchi
Wewe punga kweli nani mroho wa madaraka anaetumia majeshi kutawala ndio mroho, kuanzia kuhesabu kura unakamata watu hotelini. Chadema shida yao wafanye siasa tu hayo yakuongoza niya kijani
 
Back
Top Bottom