Patrick Elias
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 332
- 108
Kiongozi wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC, Fatou Bensouda, ameiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi ya Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta kwa muda usiojulikana.
Hii ni baada ya malalamiko kutoka kwake kuwa Kenya imekataa kushirikiana na mahakama hiyo katika kuikabidhi ushahidi unaohitajika kuendesha kesi kwa hiyo ina maana kuwa hana ushahidi wa kutosha dhidi ya Kenyatta.
Taarifa zinazohusiana
Serikali ya Kenya ilitakiwa kuikabidhi mahakama taarifa za kifedha za Rais Kenyatta pamoja na maelezo kuhusu mali yote anayomiliki.
Katika uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo Fatou Bensouda amesema kuwa hana ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka Rais Kenyatta ambaye anadaiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2007.
Zaidi ya watu 1,000 walifariki katika ghasia hizo. Bensouda amenukuliwa akisema kuwa halitakuwa jambo la busara kufutulia mbali kesi hiyo hasa ikizingatiwa kuwa Kenya haitaki kutoa ushahidi unaohitajika na mahakama hiyo.
Badala yake aliomba mahakama kuiahirisha kesi hiyo hadi pale Kenya itakapokubali kutoa ushahidi unaohitajika.
Kesi dhidi ya Kenyatta ilipaswa kuanza mapema mwezi Oktoba.
Source: BBC
http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/09/140905_kenyatta_icc_kesi.shtml
Yaani huyu mama anarukaruka tu wala hajui hii case akina ocampo, kibaki na raila waliplan waipige vipi kuwatoa kafara akina uhuru ili kibaki na raila wapone. Sasa ocampo hayuko ofisini, kibaki hayuko ofisini na raila hayuko ofisini. Na walijua raila atakuwa rais ili amalize mchezo sasa dili limebuma.