Nchi 125 wanachama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) zinakutana leo, Julai 24, 2026, katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York kupiga kura ya siri kuhusu hatma ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Karim Khan.
Karim Khan anakabiliwa na tuhuma za utovu wa maadili ya kingono, ambazo amezikanusha. Kutokana na tuhuma hizo, alisimamishwa kazi mwezi Juni 2026 baada ya Kamati ya Usimamizi ya ICC kubaini kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kazi na madai ya kujaribu kuwazuia walalamikaji kuendelea na malalamiko yao.
Soma zaidi:Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa kingono
Aidha, Khan pia alisimamishwa kwa muda katika nafasi yake ya uwakili nchini Uingereza wakati taratibu nyingine za kisheria zikiendelea.
Kwa mujibu wa taratibu za ICC, kura ya siri itahitaji angalau kura 63 kati ya nchi 125 wanachama ili kumuondoa rasmi madarakani.
Khan hakuhudhuria kikao hicho baada ya kuzuiwa kuingia nchini Marekani kufuatia vikwazo vilivyowekwa vinavyohusishwa na uchunguzi wa ICC dhidi ya viongozi wa Israel kuhusu vita vya Gaza.
Iwapo ataondolewa madarakani, ICC itaanza mchakato wa kumteua Mwendesha Mashtaka Mkuu mpya. Kwa sasa, shughuli za ofisi hiyo zinaendelea kusimamiwa na manaibu wake.
Source: Millardayo