SI KWELI Iceland mwaka 2024 ilitangaza zawadi kwa wanume watakaokwenda kuoa wananwake wa Taifa hilo

SI KWELI Iceland mwaka 2024 ilitangaza zawadi kwa wanume watakaokwenda kuoa wananwake wa Taifa hilo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Imeelezwa kuwa mwaka 2024 serikali ya Iceland iliweka sheria mpya kutokana na upungufu wa wanaume, ilikuwa inawalipa wahamiaji wa kiume $50,000 kwa mwezi iwapo wakiwaoa wanawake wa nchi hiyo

1744179448903.jpeg
 
Tunachokijua
Iceland ni nchi ya kisiwa iliyoko katika Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini. Ikiwa imepakana na Amerika ya Kaskazini na Ulaya, Iceland ni nchi yenye misimu, jiografia, na tamaduni zenye tofauti kubwa na za kuvutia. Kwa mujibu wa worldometer nchi ya Iceland ina wakazi 397,136.

Madai

Zimekuwapo taarifa zinazodai kuwa serikali ya Iceland ilianzisha sheria mpya mwaka 2024 kuwa inatoa kiwango cha shilingi dola elfu 50 kwa mwezi kwa wahamiaji wa kiume watakaowaoa wanawake wa nchi hiyo kutokana na uhaba wa wanaume nchini humo.

Uhalisia wa taarifa hiyo upoje?

JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli. Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo si ya mwaka 2024 wala 2025 na badala yake imekuwepo miaka kadhaa iliyopita.

Tovuti ya Iceland monitor mwaka 2016 ilichapisha taarifa iliyokuwa na kichwa kilichosomeka “Watu kadhaa wameamini ulaghai wa ‘Lipwa uoe wanawake wa Iceland’’, makala hiyo iliezea jinsi wizara ya mambo ya nje ya Iceland ilivyopokea maombi ya watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji nafasi hiyo ya kwenda kuoa wanawake wake wa Iceland ili kupata kiwango hiko cha fedha kilichotajwa.

Mwaka 2018 tovuti ya Iceland monitor ilichapisha tena taarifa nyingine na kueleza kuwa taarifa hizo ni za uzushi na hazina ukweli wowote. Katika taarifa yao wameinukuu wizara ya mambo ya nje ya Iceland ambayo imesisitiza kuwa taarifa zote au uvumi wowote kuhusu mpango wa kulipwa kwa ajili ya ndoa ni uzushi, na kwamba hakuna haja ya kuwasilisha maswali kwa Wizara hiyo au kwa ofisi zake za kidiplomasia.
Sipati picha wakifanya hivyo Tanzania, kina sisi kataa ndoa hata kwa $500 tu tutaoa!
 
Imeelezwa kuwa mwaka 2024 serikali ya Iceland iliweka sheria mpya kutokana na upungufu wa wanaume, ilikuwa inawalipa wahamiaji wa kiume $50,000 kwa mwezi iwapo wakiwaoa wanawake wa nchi hiyo

View attachment 3297427
Hii offer bado ipo Au imeisha. Tupeane michongo kama hii. Millioni 135 siyo hela ndogo aise
 
Aisee bei ya VISA huko ice land aisee mimi niende tu. Kufanya kazi za ndani
 
Nimeangalia vyanzo mbalimbali vya kuaminika kutoka Iceland, na ninaweza kukuhakikishia kuwa habari hiyo si ya kweli.

  1. Vyanzo vya Habari vya Iceland: Tovuti kama Iceland Monitor (mbl.is) zimeandika makala mara kadhaa (tangu mwaka 2016) zikikanusha habari hii na kuiita "hoax" (uzushi). Wanaeleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iceland ilipokea maulizo mengi kutoka kwa watu walioamini uvumi huo.
  2. Tovuti Rasmi za Serikali:
    • Tovuti rasmi ya serikali ya Iceland (kama island.is na government.is) ina sehemu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQ) ambapo wanajibu moja kwa moja kuhusu uvumi huu wakisema: "Hakuna ukweli wowote katika uvumi huu, huu ni uzushi" ("There is no truth to this rumour, this is a hoax").
    • Kurasa zinazohusu uhamiaji na vibali vya makazi kwa wanandoa katika tovuti hizi (kama zile za Directorate of Immigration) zinaelezea sheria na taratibu halisi. Hakuna mahali popote panapotajwa malipo kwa wahamiaji kuoa raia wa Iceland. Badala yake, zinaeleza masharti ya kawaida kama kuthibitisha uhalali wa ndoa, kuwa na njia za kujikimu kimaisha, na kutokuwa na ndoa za mkeka kwa lengo la kupata kibali cha makazi.
  3. Taarifa za Maafisa: Vyanzo vya habari vya kimataifa ambavyo vimefuatilia suala hili vimemnukuu Afisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iceland akithibitisha kuwa serikali hailipi watu kuhamia nchini humo.
Kwa hiyo, kwa mujibu wa vyanzo rasmi na vya kuaminika vya habari nchini Iceland, hakuna mpango wowote wa serikali wa kulipa wahamiaji pesa ili waoe wanawake wa Iceland. Ni hadithi ya uongo iliyosambaa sana mtandaoni.

Asante GEMINI
 
Back
Top Bottom