Idadi iliyosomwa na katibu na idadi ya walimu walioajiriwa ni tofauti ni

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
929
Reaction score
1,764
Nimemsikiliza kwa umakini katibu mkuu alivyokuwa akitangaza ajira za walimu waliopangiwa vituo

Katika maelezo yake amekumbushia ahadi iliyotolewa na Rais Magufuri ya kuajiri walimu zaidi ya elfu kumi na tatu.

Katika press conference, mhe. Katibu mkuu amekiri kuajiri walimu hao elfu kumi na tatu kama ilivyokuwa ahadi ya mheshimiwa Rais Magufuri.

Lakini cha kushangaza na kilicho washitua waombaji wengi ni kuwa idadi ya walimu 13,000 iliyosemwa na katibu kwenye press conference sio sawa na idadi ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi. Walimu waliopangiwa vituo roughly hawazidi elfu tisa.

Kingine kilicho washitua waombaji wengi ni mwalimu mmoja kutokea kwenye kila ukurasa na kuchukua nafasi za walimu zipatazo 195.

Kufuatia mkanganyiko huo, je kutakuwa na batch 2 ya ajira zingine kukamilisha idadi ya ajira 13,526 kama zilivyokuwa zimeahidiwa na mheshimiwa Rais?

N:B mods msiunganishe huu uzi na uzi mwingine hadi majibu yapatikane ili kuondoa wasi wasi kwa waombaji.
 
Kwani alimbiwa majina yanawekwa mara moja yote
 
Haya ndio kati ya mambo machache yanayo wafanya vijana kuichukia kozi na kazi ya ualimu.
Mungu awasaidie sana waalimu aiseeee...
And always nasemaga kwamba, "Maybe we should underpaid politicians and overpaid teachers, then they would be smarter people and less stupid laws..."
 
Bwn yule ni msanii hatari,mnao muamini endeleeni kumuamini.
 
majina yaliyoyotolewa ni elfu nane! sasa tunashindwa kuelewa tamisemi wanatuonaje
 
hayo majina wametype stationary gani maana hayajakaa kiofisi kabisa!!
 
Ukisha kula nyama ya binadamu huwezi kuwacha.
Ukidanganya kwenye Kura utaendelea kudanganya Ila sijajua Ni kwa manufaa ya Nani.
Hakuna mtu asiyejua kwamba wapinzani walipokwa ushindi.
 
Ninashauri majina yote taliyotangazwa ajira mpya za ualimu Tamisemi, zipitiwe kwanza na TISS na Takukuru kabla hawajaripoti vituo walivyopangiwa na kuanza kupewa mishahara. Kuna mchezo mchafu umechezwa na Tamisemi, jina la mtu mmoja abdalah limetokea mara 195 , wengine waliomba Wana vigezo sawa ila majina hayakutoka. Pia idadi aliyoisemwa Mh Rais sio idadi iliyotolewa.
Inasemekana Luna mwamba kumaliza form four 2019 lakini kaajiriwa au alikuwa mwalimu wa UPE akajiendeleza ?
 
Back
Top Bottom