Nimecheki Revised Edition ya Concise English-Swahili Dictionary (Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili) iliyoandikwa na R.A Snowxall and H.B. Mshindo na kuchapishwa na Oxford University Press, Dar Es Salaam, mwaka 2002.
Waandishi hao wametafsiri neno "show" kama "kuonyesha", "Maonyesho", "kujionyesha"
Pia wametafsiri neno "shown" kama "onyesha" na kulitolea mfano wa "onyesha mfano".
Katika tafsiri zote mbili hawakughusia kabisa neno "kuonesha" au "onesha"
Unaweza kusema kuwa waandishi hao wametafsiri kimakosa?
Kwa mfano, nikiandika kesho ITV "wataonyesha" Champions League live nitakuwa nimekosea?
cc.
Dingswayo