ANGALIZO; Tunapojivunia yakuwa tu "Great Thinker" hatunabudia pia kuwa makini katika uandishi, usomaji, na uhesabuji hasa juu ya Lugha yetu ya Taifa (Kiswahili).
Hili nimepata kuendelea kuliona kupitia ndani ya majukwaa (forums) ya humu JF, na linakua kwa kasi ya ajabu kadiri siku, miezi na miaka inavyojongea.
Kuna baadhi ya watu humu utakuta kama anajua Kusoma, basi hajui Kuandika, au kama anajua Kuandika basi hajui Kuhesabu au Kusoma.
Mwanzoni kipindi cha nyuma, nilidhani pengine ni mtu tu, anaweza kosea bahati mbaya katika uandishi (typing error) ila kumbe sivyo.
Mfn. Utakuta panapohitajika "r" mtu anaandika "l" au neno "Kuonesha" utakuta mtu tena na elimu yake ya kutosha tokea shule ya msingi mpaka anapata kazi anaandika au kutamka "Kuonyesha".
Au unaweza kuta panapohitajika herufi kubwa mtua anaandika ndogo.
Na hili ni kwa upande wa Lugha yetu ya Taifa (Kiswahili), upande wa Lugha nyingine nahofu kuliongelea maana hata mimi si mjuzi nazo.
Kwa anayebisha au wale wepesi wakuulizia neno "SOURCE", anza na hoja za wachangiaji humu humu....!
ANGALIZO; Tunapojivunia yakuwa tu "Great Thinker" hatunabudia pia kuwa makini katika uandishi, usomaji, na uhesabuji hasa juu ya Lugha yetu ya Taifa (Kiswahili).
Nitakuwa nimekosea kama nikisema na wewe ni wale wale?
Lipi neno sahihi kati ya "kuonesha" na "kuonyesha"?
Kuna baadhi ya watu humu utakuta kama anajua Kusoma, basi hajui
Kuandika, au kama anajua Kuandika basi hajui Kuhesabu au Kusoma.
Hivi wewe mtoa mada,ulifikiria kweli?Inawezekana vipi mtu ajue kuandika halafu asiweze kusoma?..
kama umeshindwa kutofautisha kati ya mwenye ulemavu wa kuona na mwenye makengeza basi si makosa yangu. Ila siwezi KUKUONYA, ila naweza KUKUONESHA.
Haya bana. Wapo walioanzisha mpaka thread juu ya matumizi ya haya maneno: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/125825-kuonesha-au-kuonyesha.html
Neno "kuonyesha" nimefundishiwa tokea nikiwa shule ya msingi kuwa ni sahihi.
Bado siamini kuwa wewe upo sahihi na mwalimu wangu wa primary alikuwa wrong.
I'm sure Dingswayo, Chamoto, Nyani Ngabu Gaijin "watatuonyesha" njia.
Ni "maonyesho" au "maonesho" ya mavazi?
Haya bana. Wapo walioanzisha mpaka thread juu ya matumizi ya haya maneno:
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/125825-kuonesha-au-kuonyesha.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/101110-tofauti-kati-ya-onesha-na-onyesha.html
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/27556-ni-onesha-au-onyesha.html
Neno "kuonyesha" nimefundishiwa tokea nikiwa shule ya msingi kuwa ni sahihi.
Bado siamini kuwa wewe upo sahihi na mwalimu wangu wa primary alikuwa wrong.
I'm sure Dingswayo, Chamoto, Nyani Ngabu Gaijin Justin Byabato, Tukufu, Ntaramuka, Maamuna, "watatuonyesha" njia.
Ni "maonyesho" au "maonesho" ya mavazi?
Kiswahili sanifu ni 'kuonyeshwa' litokalo na neno la tendo 'onyesha'. Hata hivyo neno 'onesha' inatumiwa pia na baadhi ya watu katika lahaja zao na hivyo kuonekana kwao kuwa ni sahihi.
mkuu, maneno yote yapo sahihi, ila inategemea unalitumia wapi ili lilete maana sahihi iliyokusudiwa.
Tuko pamoja mkuu.Hili nimepata kuendelea kuliona kupitia ndani ya majukwaa (forums) ya humu JF, na linakua kwa kasi ya ajabu kadiri siku, miezi na miaka inavyojongea.
Kuna baadhi ya watu humu utakuta kama anajua Kusoma, basi hajui Kuandika, au kama anajua Kuandika basi hajui Kuhesabu au Kusoma.
Mwanzoni kipindi cha nyuma, nilidhani pengine ni mtu tu, anaweza kosea bahati mbaya katika uandishi (typing error) ila kumbe sivyo.
Mfn. Utakuta panapohitajika "r" mtu anaandika "l" au neno "Kuonesha" utakuta mtu tena na elimu yake ya kutosha tokea shule ya msingi mpaka anapata kazi anaandika au kutamka "Kuonyesha".
Au unaweza kuta panapohitajika herufi kubwa mtua anaandika ndogo.
Na hili ni kwa upande wa Lugha yetu ya Taifa (Kiswahili), upande wa Lugha nyingine nahofu kuliongelea maana hata mimi si mjuzi nazo.
Kwa anayebisha au wale wepesi wakuulizia neno "SOURCE", anza na hoja za wachangiaji humu humu....!
ANGALIZO; Tunapojivunia yakuwa tu "Great Thinker" hatunabudia pia kuwa makini katika uandishi, usomaji, na uhesabuji hasa juu ya Lugha yetu ya Taifa (Kiswahili).
Katika kamusi yangu ya Johnson and Madam iliyochapishwa mara ya kwanza mwaka 1939 ..
Nimecheki Revised Edition ya Concise English-Swahili Dictionary (Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili) iliyoandikwa na R.A Snowxall and H.B. Mshindo na kuchapishwa na Oxford University Press, Dar Es Salaam, mwaka 2002.
Waandishi hao wametafsiri neno "show" kama "kuonyesha", "Maonyesho", "kujionyesha"
Pia wametafsiri neno "shown" kama "onyesha" na kulitolea mfano wa "onyesha mfano".
Katika tafsiri zote mbili hawakughusia kabisa neno "kuonesha" au "onesha"
Unaweza kusema kuwa waandishi hao wametafsiri kimakosa?
Kwa mfano, nikiandika kesho ITV "wataonyesha" Champions League live nitakuwa nimekosea?
cc. Dingswayo
Baraza la Kiswahili la Taifa huandaa na kutoa machapisho yanayoonyesha kazi mbalimbali. Baadhi ya machapisho ni:
BAKITA hushiriki kwenye maonyesho mbalimbali ya Vitabu ili kutangaza kazi, na bidhaa za BAKITA yakiwemo machapisho. Maonyesho hayo ni pamoja na:
Mkuu, hili naunga mkono.
Hawa jamaa lazima watakuwa wanakosea kila mwaka.