Idadi ya fimbo anazotakiwa kuchapwa mwanafunzi

Idadi ya fimbo anazotakiwa kuchapwa mwanafunzi

Wana JF naomba kujuzwa, kwa anayefaham kiwango cha fimbo, anachotakiwa kuchapwa mwanafunzi pindi anapofanya kosa shuleni? Maana huku kwetu st kayumba naona kumchapa mwanafunzi imekua fashion..utakuta kijana anachapwa hadi anaichukia shule.

Natanguliza shukran wana jamvi

wewe kama ni mzazi tumia busara kwenye sana kwenye hilo swala. Maana unaweza kusimama upande wa mwanao kumbe ni mkorofi sana shuleni. Na mzazi ukisha kuwa unamtetea hivyo mwanao unamtengenezea mazingira ya kufeli maana utakuwa unaanzisha mgogoro na walimu. Maana jua uki anza mgogoro na mwalimu mmoja ni sawa na kuingia mgogoro na staff nzima, yaani ni kama polisi ukikosana na mmoja basi unapata shida na wote. Na atakaye umia hapo ni mwanao maana hao hao walimu ndio wana dhamana ya mwanao kitaaluma ukiwatibua ni rahisi sana kumfelisha mwanao hata kumuandikia ripoti chafu baraza la mtihani ambayo itamfelisha

ushauri fuatilia kosa la mwanao lililo sababisha achapwe ili ujue chanzo. Coz unaweza kumtetea kumbe kosa lake lilikuwa la kufukuzwa shule ila mwalimu kaona amuadhibu yaishe,halafu mtoto akaja kwako kukueleza uongo utakao mlinda yeye ili aonekane hana hatia. so tumia busara tu kwa hli ili usimuumize mwanao kitaaluma achana na hao wanao jifanya wanasheria poli wakati hawana hakika na wanacho kueleza maana nao wamesikia mitaani . Kuhusu idadi ya viboko kwa mujibu wa sheria visizidi 6 kwa kosa kubwa . Na zaidi ni mtoto kurudishwa nyumbani hadi hapo bodi ya shule itakapo kaa,
 
wewe mzazi unajifanya una akili sn na ukitaka mtt wako aharibike endelea kumtetea kwa mambo ya kipumbavu eti asipigwe bakora mtoto wakiafrika km unaona anaposoma mpeleke ambako hawachapi au kaa naye nyumbani kwako mfundishe,ONDOA HOJA ZA KIJINGA HAPA UNATUMALIZIA BANDO TU
 
Awali ya yote mkuu,kati adhabu ngumu kama kung'oa viski, mawe na kadhalika kipi kwa mtazamo wako ungeonelea kifanyike,kwa uzoefu,mwanafunzi wa o'level anatakiwa kuchawa fimbo 4 tu kwa kosa moja,ila mkuu wa shule ndo anatakiwa aruhusu mwanafunzi huyo aadhibiwe,KWA UPANDE wa A'LEVEL mwanafunzi anatakiwa kuchapwa fimbo 2 kwa kosa moja,ila mkuu wa shule ndiye atoaye adhabu hiyo na siyo mwalimu mwingine!!

mkuu umesema A level mwisho fimbo 2 iyo ndo sheria au? Maana naona uku mkoani kunashule kongwe tu ila wanapiga mpaka wanafunzi wanaihama iyo shule
 
Fimbo napendekeza ziwepo .. chapa hao.. kuna watu wapo mashuleni ila ktabia unabidi wawe magarezani.. sas awewe hao unawasaidiaje.. FIMBO ZIWEPO
 
Fimbo huwa mwisho tatu..sema ubinadam unapitiliza kwa kosa analofanya mwanafunzi
 
Back
Top Bottom