Idadi ya Mawakili Tanzania hadharani

Idadi ya Mawakili Tanzania hadharani

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania imetoa Orodha Kamili ya Mawakili Wasomi Tanzania Bara ambao wamekubaliwa na kusajiliwa hadi sasa.

Nyaraka hiyo yenye kichwa 'Roll of Advocates' inaonesha kuwa Tanzania,yenye watu takribani milioni 45, ina jumla ya Mawakili Wasomi 3626.


Nyaraka husika inaonesha kuwa Mawakili wa mwisho kusajiliwa ni wale wa tarehe 21/6/2013. Nyaraka hiyo imetolewa baada ya Ofisi husika kufanya marekebisho katika Orodha hiyo kwa kuwatoa Mawakili Wasomi ambao wameshafariki.

Kuanzia mwaka 2008, Mwanasheria yeyote anayehitaji kuwa Wakili lazima asome na kufaulu Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo katika Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo Tanzania almaarufu kama 'Law School of Tanzania'.

Kuna kila sababu kwa wahusika wote wa kuandaa na kukubali Mawakili kufanya juhudi za makusudi kuongeza idadi ya Mawakili nchini. Iliyopo sasa haitoshi kwa kweli.

Kwa idadi iliyopo sasa,watu wengi watakosa huduma za Mawakili Wasomi ambao wengi wameng'ang'ania Dar es Salaam.


Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Ni kweli kabisa idadi kubwa ya mawakili ipo hapa jijini Dar es salaam na hivyo kufanya idadi kubwa ya wananchi kukosa msaada wa kisheria.Ili kupata msaada wa kisheria inawalazimu watumie gharama nyingi sana kuwapata mawakili ikiwemo hii ya usafirishaji kutoka Dar kwenda sehemu nyingine za Tanzania bara.

Kwa rehema za mwenyezi Mungu atanijalia na huenda nkawa mmoja wa wakili katika wilaya ya Tarime mkoani Mara

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom