Kwa mtazamo wangu, ninaona miaka 10 ijayo idadi ya single parents itaongezeka mara dufu ukilinganisha na kipindi kilichopita kuanzia miaka ya 90 kurudi nyuma. Kwa miaka hiyo, wanandoa walikuwa wanapatana kuishi pamoja hasa baada ya kupendana.
Dhana kuu ya umoja wa ndoa ilikuwa ni kuishi bila kutengana mpaka pale kifo kinapowatenganisha. Changamoto za ndoa zilikuwepo lakini bado ndoa ziliendelea kuwa imara kwa sababu tu, ndoa ilijengwa katika upendo.
Miaka ya hivi karibuni tunapitia katika changamoto kubwa sana ya mahusiano ya ndoa. Akili zetu zinaangazia ni yupi ana kipi au anamiliki nini au ana kazi gani ili michakato ya ndoa ifanyike. Tuangaliii tena zao la ndoa ambalo ni upendo bali matamanio ya mali na utajiri.
Vitu hivi vinapokwisha, ndoa nyingi huwa katika hatari ya kuvunjika na kuwaacha watoto wakiishi na mzazi mmoja au pengine kukosa malezi ya wazazi kabisa. Mitandaoni huku ndio hatari kabisa. Tunatafuta wenza huku tukiwa na masharti lukuki ya tamaa ya mali, ajira na mionekano bandia.
Tamaa zetu hizi tunaziweka mbele pengine bila kutambua kwamba ndoa hujengwa katika misingi ya upendo na maelewano baina ya mke na mme ambao wana kiu ya kujenga familia pamoja.
MAONI YANGU: Tubadilishe mtazamo juu ya vigezo vya kuanzisha mahusiano ya uchumba na ndoa. Tukifanya hivi, single mothers/fathers watapungua.
Yule graduate pale ambae hana kazi wala mchongo wowote atamuoa mwanamke wa maisha yake na ndoa itadumu hadi kifo.
Yule kaka pale ambae hana kazi atampata mwanamke anaempenda pia. Yule mama/dada ambae hana kazi atampata mwanaume ambae hataweza kuangalia status yake ya maisha na ndoa yao itadumu katika upendo.