Idadi ya SMS ndani ya nchi imeongezeka kutoka SMS bilioni 52.8 mwezi Juni 2025 hadi kufikia bilioni 52.9 mwezi Septemba 2025 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.2.
Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano ya robo mwaka inayoishia Septemba 2025 inaonesha kuwa Mwezi Septemba 2025 ulikuwa na idadi kubwa ya SMS ikilinganishwa na miezi mingine kwenye kipindi husika.
💡Ripoti hiyo hutolewa kila robo mwaka kwa lengo la kuonyesha mwenendo wa ukuaji wa sekta ya mawasiliano na inapatikana pia kupitia tovuti ya TCRA.🎯
Tembelea tovuti ya TCRA (www.tcra.go.tz ) kwenye kipengele cha Machapisho, kisha bofya Takwimu, au bofya kiunganishi https://bit.ly/48CADOW ili kusoma ripoti nzima ya Sekta ya Mawasiliano (Julai – Septemba 2025).
Kutokana na Mvutano uliopo kati ya Serikali, Watoa Huduma na Wananchi kuhusu Bundles na Shutuma za Wizi inabidi sisi wananchi tuelewe tunataka nini na Wizi ni nini?
Issue za Wizi:
Kama kuna issue za Wizi na mtu kaibiwa kuna vyombo vya kisheria na TCRA inabidi mwananchi aweze kupeleka issue zake huko ili asaidiwe, na hapa wizi ni kuuziwa tofauti na makubaliano yaani unanunua mb 10 unapewa mbili na sio gharama ya bei
SULUHISHO
A: Serikali ikae Kando
Mbaya katika haya mambo mara zote ni Serikali kuingilia haya mambo na mara nyingine gharama inatokana na Tozo / Au Sheria za...