Miaka 39 iliyopita wakati Nyerere anaondoka madarakani aliacha kiwanda cha kuunganisha maroli ya Scania na matrekta ya Valmet kule kibaha. Halafu kulikuwa na kiwanda cha kutengeza mabodi ya mabasi na marali cha Quality Garage (ambachpo nadhani kilikuwa cha Ukoo wa Manji). Vile vile nadhani kulikuwa na kiwanda kingine cha kufunga magari ya aina ya TATA .
Baada ya hapo nchi ilisismamama kabisa kiviwanda ikawa ni ya kutegemea misaada, mikopo na kubinafsisha viwanda alivyoacha Nyerere. Nyerere alianzisha viwanda vya nguo vingi sana, lakini Mkapa akavibinafsisha kwa bei karibu na bure: Ninavyoweza kukumbuka ni pamoja Mutex, Mwatex, Tabotex, Polytex, Canvass, Urafiki, Kiltex, Sungura textiles, .....