Idadi ya wabunge tarajiwa ACT-Wazalendo inawabeba dhidi ya CHADEMA Bungeni, kama Zitto akishinda Ubunge kuwa KUB

Idadi ya wabunge tarajiwa ACT-Wazalendo inawabeba dhidi ya CHADEMA Bungeni, kama Zitto akishinda Ubunge kuwa KUB

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Hii inatokana na uzoefu wa kura za Wazanzibar hususani wapemba ambao hupiga kura kutegemea chama anachotoka Maalim Seif. Kama hali itakuwa hivyo ACT wana uhakika wa wabunge angalau 20 kutoka Zanzibar kitu ambacho CHADEMA au chama kingine hakiwezi kupata wabunge kumi (10) nchi nzima.

Kwa siasa za kibunge zilivyo; chama cha upinzani chenye wabunge wengi bungeni ndicho chenye mamlaka ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni na kwa kuzingatia turufu ACT-Wazalendo wanayotarajia haswa kuwa na wabunge toka Zanzibar ni dhahiri wataongoza upinzani bungeni na kama Zitto akishinda ubunge basi ni KUB ajaye.

Uhalisia ulivyo ni kwamba baadhi ya wabunge wa CHADEMA walimaliza muda wao wameonekana kutumia turufu ya umaarufu wao na ''ustaafu'' (incumbency) kwenye kampeni lakini ''vote dynamics' zinawakataa na hapa ndipo ninampongeza kijana wangu John Mnyika aliyesoma alama za nyakati vema baada ya kuona kiza mbeleni na kuamua kustaafu siasa za bungeni.

Namuona Tundu Lissu akiweka nguvu angalau kupata wabunge na hatimaye kura ambazo zitasaidia kupata ruzuku na fursa ya u-KUB lakini hali ni tete sana kulingana na uhalisia uliopo

Hoja kwa hoja, utafiti kwa utafiti.
 
Wabunge wa Pemba watako ingia bungeni ni wachache Bado CDM inanafasi ya kuendelea kuwa na wabunge wengi kwenye bunge la JMT.
 
Nini faida ya uwepo wa KUB, na anatakiwa awe na sifa zipi?
 
Duuh,mmeshawakataa NCCR mageuzi na sasa mnahaha na kurukaruka!Ile ya kusema NCCR ndio watakuwa chama kikuu cha upinzani imeishia wapi?
Safari hii CCM jiandaeni kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni!
 
We 'kimbelembele' chako kitakuponza, boss yupo Kigoma alafu unampa ZZK turufu ya Ubunge mezani na yeye alisema hataki kuwekewa 'gunzi' kwenye tochi......
Utakosa vyote..... Be advised.
 
Nilifikiri KUB wenu wa kutengeneza alikua mzee wa Mama Tanzania! Gear imebadilikia wapi?!
Ndo ujue maji yameshazidi unga. Walipambana sana kuhusu mama tanzagiza kuwa kub.
Wameona biashara yao imebuma wamehamia kwa Zitto, baada ya hapo wataanza kujifariji kwamba ikulu wataikosa lkn watakuwa na kub bungeni.
Kwa heri mkononi mweusi "ccm"

Sent from my Infinix X606B using JamiiForums mobile app
 
namhurumia sana mpinzani wa kweli na mtu makini kama maalim seif kujiingiza kwenye hikii chama cha ma-snitch act wazalendo, sipati picha atakuaje pale atakapo uzwa kwa wakoloni weusi ccm...
 
Sioni uwezekano wa jambo hilo kutokea,,ukweli ni kwamba CHADEMA wana uhakika wa kushinda si pungufu ya majimbo 20 pia watapata wabunge wengi wa viti maalum kwa kuzingatia idadi ya kura za urais.

ACT nj kweli watapa wabunge karibu 20 kutoka Zanzibar lakini sioni wakipata zaidi ya wabunge 4 bara,pia hawatapata idadi ya kutosha ya wabunge wa viti maalum.Kwa vyovyote vile CHADEMA kama watashindwa uchaguzi basi ndo kitaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani baada ya uchaguzi huu.Kwa upande wa ACT wana future nzuri 2025.
 
Hizi story tulishazizoea ndugu
Furaha yenu mnataka cdm ife kitu ambacho mmeshafail, sasa hivi mmebakia kuotea tu , cdm wanaenda kuongeza idadi kubwa sana ya majimbo bara yaani uku kitaa ccm mmebakia kuliwa viela vyenu tu but in reality mnapulia mashine
 
namhurumia sana mpinzani wa kweli na mtu makini maalim seif kujiingiza kwenye hikii chama cha ma-snitch act wazalendo, sipati picha atakuaje pale atakapo uzwa kwa wakoloni weusi ccm...
Baada ya uchaguzi, ccm itaondoka, alafu kutakua na muungano mpya kabisa kwenye jamuhuri yetu! Pia naona chama kipya, Maalim akiwakilisha Zenji na CHADEMA bara! (Maalim hategemei chama chochote, chama kinamtegema, hasa Zanzibar!)
 
CHADEMA sidhani kama wanataka kuwa Chama kikuu cha upinzani.

CHADEMA wana lengo la kushinda uchaguzi na kushika Dola.

NI YEYE.
 
Back
Top Bottom