Idadi ya wabunge tarajiwa ACT-Wazalendo inawabeba dhidi ya CHADEMA Bungeni, kama Zitto akishinda Ubunge kuwa KUB

Idadi ya wabunge tarajiwa ACT-Wazalendo inawabeba dhidi ya CHADEMA Bungeni, kama Zitto akishinda Ubunge kuwa KUB

Namuona Tundu Lissu akiweka nguvu angalau kupata wabunge na hatimaye kura ambazo zitasaidia kupata ruzuku na fursa ya u-KUB lakini hali ni tete sana kulingana na uhalisia uliopo
chadema hawapati hata wabunge watano
 
Ndugu zangu,

Hii inatokana na uzoefu wa kura za Wazanzibar hususani wapemba ambao hupiga kura kutegemea chama anachotoka Maalim Seif. Kama hali itakuwa hivyo ACT wana uhakika wa wabunge angalau 20 kutoka Zanzibar kitu ambacho CHADEMA au chama kingine hakiwezi kupata wabunge kumi (10) nchi nzima.

Kwa siasa za kibunge zilivyo; chama cha upinzani chenye wabunge wengi bungeni ndicho chenye mamlaka ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni na kwa kuzingatia turufu ACT-Wazalendo wanayotarajia haswa kuwa na wabunge toka Zanzibar ni dhahiri wataongoza upinzani bungeni na kama Zitto akishinda ubunge basi ni KUB ajaye.

Uhalisia ulivyo ni kwamba baadhi ya wabunge wa CHADEMA walimaliza muda wao wameonekana kutumia turufu ya umaarufu wao na ''ustaafu'' (incumbency) kwenye kampeni lakini ''vote dynamics' zinawakataa na hapa ndipo ninampongeza kijana wangu John Mnyika aliyesoma alama za nyakati vema baada ya kuona kiza mbeleni na kuamua kustaafu siasa za bungeni.

Namuona Tundu Lissu akiweka nguvu angalau kupata wabunge na hatimaye kura ambazo zitasaidia kupata ruzuku na fursa ya u-KUB lakini hali ni tete sana kulingana na uhalisia uliopo

Hoja kwa hoja, utafiti kwa utafiti.
Upinzani hautazidi wabunge wa kuchaguliwa 10! Wajiandae kwa maumivu tu.
 
Back
Top Bottom