Mufti kuku The Infinity
JF-Expert Member
- Sep 21, 2019
- 6,053
- 10,032
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) na taasisi nyingine za utafiti, idadi ya Waislamu duniani inakadiriwa kufikia zaidi ya bilioni 2.
Kwa sababu ya kiwango cha juu cha uzazi na kasi ya kuenea kwa dini hiyo kwenye maeneo mengi duniani, inatarajiwa kuwa idadi ya Waislamu itaongezeka hadi kufikia bilioni 3.3 ifikapo mwaka 2060.
Sababu nyingine ya ukuaji wa Uislamu ni kuongezeka kwa idadi ya Waislamu wanaoongoka kutoka dini nyingine, pamoja na idadi kubwa ya Waislamu wanaozaliwa.
Aidha, kuenea kwa kiwango cha juu cha teknolojia na mawasiliano ya kijamii yamekuwa na athari kubwa katika kuenea kwa dini hiyo, kwani inakuwa rahisi kwa watu kufikia na kusambaza ujumbe wa Kiislamu kote duniani.
Mwenyezimungu tunakuomba uwape baraka wote wanao fanikisha kuenea kwa hiu dini yako tukufu, vilevile waongoze wote ambao hawapo kwenye uislamu waweze kuingia kwenye dini hii ya haki. Aamin 🙏🏻🤲🤲