Idadi ya wakimbizi wa Ukraine kufikia milioni 1.5

Idadi ya wakimbizi wa Ukraine kufikia milioni 1.5

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mashambulio ya Urusi dhidi ya Ukraine yaingia katika siku ya 11 huku idadi ya wakimbizi ikitarajiwa kufikia karibu watu milioni 1.5. Mataifa hayo yametupiana lawama kuhusu kukwama kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Idadi ya wakimbizi wa Ukraine inatarajiwa kufikia watu milioni 1.5 huku Urusi ikiendelea na mashambulizi yake ambayo leo Jumapili Machi 6, yameingia siku ya 11.

Moscow na Kyiv wameendelea kutupiana lawama juu ya kushindikana kwa mpango wa kusitisha mapigano ambao ungeruhusu raia kuondoka kutoka kwenye miji ya Kusini iliyozingirwa na vikosi vya Urusi ya Mariupol na Volnovakha.

Raia wa Ukraine waliofanikiwa kuondoka wameingia katika nchi jirani za Poland, Romania, Slovakia na maeneo mengine.

Duru nyingine ya mazungumzo kati ya pande mbili hizo imepangwa kufanyika Jumatatu Machi 7, 2022.

Katika hotuba ya jana, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy alitoa wito kwa watu wake walio kwenye maeneo yanayokaliwa na jeshi ya Urusi kuendelea kupambana. Amesema ni lazima Waukraine wapambane kuuondoa uovu wa Urusi katika miji yao, akitoa ahadi ya ya kulijenga upya taifa lake.

Rais Zelensky amesema amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Marekani, Joe Biden na walijadili juu msaada wa fedha pamoja na vikwazo-zaidi dhidi ya Urusi katika kipindi hiki ambacho taifa lake linakabiliwa na ongezeko la mashambilizi.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett amekutana na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Berlin kwa lengo la kumpa taarifa ya mazungumzo yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Hebestreit amesema Bennett na Scholz wamekubaliana kuwa na mawasiliano ya karibu na kwamba lengo lao kubwa ni kuvimaliza vita vya Ukraine, haraka iwezekanavyo.

Rais wa Urusi Vladmir Putin alionya siku ya Jumamosi kwamba nchi yoyote itakayochukua hatua ya kuifunga anga ya Ukraine itazingatiwa na Moscow kuwa imeingia kwenye mzozo huo.

Kiongozi wa Ukraine Volodymyr Zelensky anazitaka nchi za Magharibi kuunga mkono hatua za kuifunga anga yake ili kuminunga mkono nchi yake inayoshambuliwa na Urusi lakini washirika wake hadi sasa wamepinga hatua hiyo, wakihofia kuwa itazidisha vita na Urusi yenye silaha za nyuklia.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya NATO, Jens Stoltenberg na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken wote wametoa kauli hiyo ya kukataa kuchukuliwa hatua za kuifunga anga katika ukanda wa Ukraine licha ya maombi ya mara kwa mara ya Ukraine nchi hiyo ya kutaka kuwekwa marufuku ya ndege kuruka kwenye anga yake.

Source: RTR/AFP/DPA

61030570_401.jpg
 
Russia haamini macho yake, yeye alifikiri ingekuwa kama kumsukuma mlevi sasa gemu imekuwa ngumu na isiyotabirika. Masaa 24 waliyotabiri kwamba yangewatosha kuiteka Ukraine sasa ni majuma yanakatika.

Kuna askari wa Russia hawana ari ya kupigana kwenye hivi vita hadi makamanda wao kwani kabla ya uvamizi kuna makamanda ambao hawakuafiki vita.

Kiujumla, hatima ya hivi vita lazima utawala wa Putin uathirike na lazima Russia watalazimishwa kulipa gharama zote za vita na uharibifu ambao watakuwa wamefanya Ukraine ikiwa kama sharti la kuja kuondolewa vikwazo vikali walivyowekewa.
 
Back
Top Bottom