Ndugu zangu nimekuwa nikihisi kuwepo kwa ubabaishaji mkubwa katika Tume ya Uchaguzi, awali walituambia wapiga kura wamefikia milioni 21, baadae wakasema wamefanya marekebisho sasa wapiga kura ni milioni 19 na ushee. Kweli juzi nilipoingia kwenye tovuti yao nikaona idadi hiyo ingawa yana kichwa cha uboreshaji wa awamu ya kwanza kwa mwaka 2007-2008, lakini cha kushangaza leo nimefungua tovuti yao nakutana na idadi hii 18,014,667.
Swali je inawezekana tume haijui idadi kamili ya wapiga kura ?
Na Kama ndio basi kunahaja gani ya kufanya uchaguzi bila ya kujua idadi ya wapiga kura.