Idara ya elimu sekondari Bagamoyo ina kila uozo wa rushwa katika maeneo mbalimbali. Rushwa hizo zimejidhihirisha katika maeneo yafuatayo: 1.Kupangiwa kituo cha kazi: Ili mwalimu apangiwe katika eneo zuri la kazi analazimika kutoa chochote kwa Afisa mhusika.Kwa walimu wa kike wanalazimika mpaka kutoa rushwa ya ngono.Utaona shule moja ya mjini ina walimu wengi wa kike.Wale wasiokuwa na chochote hupangiwa vijijini.Wakati mwingine walimu hutumia ndugu zao wakubwa ili wapangiwe mjini. 2.Mishahara hewa:Kuna baadhi ya walimu watoro hata miezi sita wanapata mishahara wakiwa hawafiki kazini.Wanatoa rushwa kwa wakuu wa shule na Afisa Elimu sekondari ili wawalinde.Walimu hawa wamekuwa wakilipwa mishahara wasiyo ifanyia kazi.Wengine wameajiriwa kabisa katika shule za private huku wakiacha kabisa kufanya kazi katika shule zao walizoapangiwa na serikali.Hali hii imekuwa ikidhorotesha elimu kwa kiasi kikubwa. 3.Kupata ruhusa ya kwenda masomoni.Ili mwalimu apate ruhusa ya kwenda masomoni wakati mwingine analazimika kutoa rushwa ili apate ruhusa.Walimu wasiotoa rushwa wananyimwa ruhusa kwa sababu mbalimbali. 4.Kupanda kwa madaraja. Kuna baadhi ya walimu wana miaka mingi bila ya kupandishwa madaraja.Ili mwalimu apandishwe daraja kwa wakati analazimika kutoa rushwa.Hata upandishaji wa madaraja ni rushwa tupu na kujuana. 5.Fursa mbalimbali ktk ualimu (Kwenda semina,kwenda kusahihisha mitihani ya kitaifa na kusimamia mitihani ya kitaifa f2,f4 na f6.Hapa ndo kuna uvundo wa hali ya juu.Rushwa na kujuana kuko nje nje.Kuna walimu wamejenga uswahiba na urafiki wa hali ya juu na mabosi wa idara ya elimu sekondari.Walimu hawa wanapewa fursa mbalimbali kwa kuwa wametoa rushwa au wanafahamiana na mabosi wa idara ya elimu.Unakuta mwalimu mmoja kwenye kusimamia mtihani wa f2 yumo,mtihani wa f4 yumo na mtihani wa f6 yumo kwa kuwa ametoa rushwa au anafahamiana na Afisa Elimu au na mtendaji katika ofisi ya elimu.Mwalimu huyo huyo kila mwaka hakosi kwenda kusimamia mitihani ya kitaifa wakati kuna walimu wanasifa kama zake lakini hawateuliwi kwenda kusimamia ati kwa kuwa wamegoma kutoa rushwa kwa wakuu wa shule au kwa Afisa elimu na wasaidizi wake.Hali hii imepelekea kwa baadhi ya walimu kuvunjika moyo wa kufundisha na baadhi yao wamesikika wakisema watahama katika vituo vyao vya kazi au kuasi kwa kutofanya kazi kabisa.Uozo huu wa ubaguzi,rushwa na kujuana umedhihirika katika shule karibuni zote za Bagamoyo.Shule zilizokubuhu na uozo huu wa rushwa na kujuana katika kazi maalum ni shule ya sekondari Kingani,shule ya sekondari Matimbwa,shule ya sekondari Kiromo,shule ya sekondari Dunda,shule ya sekondari Bwawani,shule ya sekondari Bagamoyo na shule ya sekondari Zinga. Mfano kuna mtumishi mmoja katika idara ya elimu sekondari amekithiri kwa vitendo hivi vya rushwa,baadhi ya walimu wa kike wamekuwa wakimpa rushwa ya ngono ili awapange katika kazi maalum kama kusimamia mitihani.Hali hii ikiachiliwa iendelee walimu wanaonyimwa fursa katika kazi maalum wanaweza wakaleta athari kubwa kama kufanya kazi chini ya kiwango na kuleta migogoro kazini.Hata hivyo sheria za kazi zinapinga matabaka na ubaguzi mahali pa kazi.PCCB mmelala?