Idara ya elimu Bagamoyo na kashfa ya rushwa

Idara ya elimu Bagamoyo na kashfa ya rushwa

mbeyaman

Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
97
Reaction score
28
Idara ya elimu sekondari Bagamoyo ina kila uozo wa rushwa katika maeneo mbalimbali. Rushwa hizo zimejidhihirisha katika maeneo yafuatayo: 1.Kupangiwa kituo cha kazi: Ili mwalimu apangiwe katika eneo zuri la kazi analazimika kutoa chochote kwa Afisa mhusika.Kwa walimu wa kike wanalazimika mpaka kutoa rushwa ya ngono.Utaona shule moja ya mjini ina walimu wengi wa kike.Wale wasiokuwa na chochote hupangiwa vijijini.Wakati mwingine walimu hutumia ndugu zao wakubwa ili wapangiwe mjini. 2.Mishahara hewa:Kuna baadhi ya walimu watoro hata miezi sita wanapata mishahara wakiwa hawafiki kazini.Wanatoa rushwa kwa wakuu wa shule na Afisa Elimu sekondari ili wawalinde.Walimu hawa wamekuwa wakilipwa mishahara wasiyo ifanyia kazi.Wengine wameajiriwa kabisa katika shule za private huku wakiacha kabisa kufanya kazi katika shule zao walizoapangiwa na serikali.Hali hii imekuwa ikidhorotesha elimu kwa kiasi kikubwa. 3.Kupata ruhusa ya kwenda masomoni.Ili mwalimu apate ruhusa ya kwenda masomoni wakati mwingine analazimika kutoa rushwa ili apate ruhusa.Walimu wasiotoa rushwa wananyimwa ruhusa kwa sababu mbalimbali. 4.Kupanda kwa madaraja. Kuna baadhi ya walimu wana miaka mingi bila ya kupandishwa madaraja.Ili mwalimu apandishwe daraja kwa wakati analazimika kutoa rushwa.Hata upandishaji wa madaraja ni rushwa tupu na kujuana. 5.Fursa mbalimbali ktk ualimu (Kwenda semina,kwenda kusahihisha mitihani ya kitaifa na kusimamia mitihani ya kitaifa f2,f4 na f6.Hapa ndo kuna uvundo wa hali ya juu.Rushwa na kujuana kuko nje nje.Kuna walimu wamejenga uswahiba na urafiki wa hali ya juu na mabosi wa idara ya elimu sekondari.Walimu hawa wanapewa fursa mbalimbali kwa kuwa wametoa rushwa au wanafahamiana na mabosi wa idara ya elimu.Unakuta mwalimu mmoja kwenye kusimamia mtihani wa f2 yumo,mtihani wa f4 yumo na mtihani wa f6 yumo kwa kuwa ametoa rushwa au anafahamiana na Afisa Elimu au na mtendaji katika ofisi ya elimu.Mwalimu huyo huyo kila mwaka hakosi kwenda kusimamia mitihani ya kitaifa wakati kuna walimu wanasifa kama zake lakini hawateuliwi kwenda kusimamia ati kwa kuwa wamegoma kutoa rushwa kwa wakuu wa shule au kwa Afisa elimu na wasaidizi wake.Hali hii imepelekea kwa baadhi ya walimu kuvunjika moyo wa kufundisha na baadhi yao wamesikika wakisema watahama katika vituo vyao vya kazi au kuasi kwa kutofanya kazi kabisa.Uozo huu wa ubaguzi,rushwa na kujuana umedhihirika katika shule karibuni zote za Bagamoyo.Shule zilizokubuhu na uozo huu wa rushwa na kujuana katika kazi maalum ni shule ya sekondari Kingani,shule ya sekondari Matimbwa,shule ya sekondari Kiromo,shule ya sekondari Dunda,shule ya sekondari Bwawani,shule ya sekondari Bagamoyo na shule ya sekondari Zinga. Mfano kuna mtumishi mmoja katika idara ya elimu sekondari amekithiri kwa vitendo hivi vya rushwa,baadhi ya walimu wa kike wamekuwa wakimpa rushwa ya ngono ili awapange katika kazi maalum kama kusimamia mitihani.Hali hii ikiachiliwa iendelee walimu wanaonyimwa fursa katika kazi maalum wanaweza wakaleta athari kubwa kama kufanya kazi chini ya kiwango na kuleta migogoro kazini.Hata hivyo sheria za kazi zinapinga matabaka na ubaguzi mahali pa kazi.PCCB mmelala?
 
Pole sana. Najua umeumia kwa kiasi kikubwa. Nimesikitishwa sana na taarifa hiyo. Hali hiyo imekithiri katika shule nyingi za sekondari hapa TZ. Nimeshashuhudia mara nyingi walimu fulani hawakosi kwenda kusimamia mitihani, kusahihisha na kuhudhuria semina, hata kama semina hizo haziwahusu, mfano mkuu wa shule/makamu wanakwenda kwenye semina ya MICHEZO wanamwacha mwalimu wa michezo shuleni. Nimegundua maafisa elimu na wakuu wa shule wengi ni kikwazo kwa walimu. ADUI WA MWALIMU NI MWALIMU MWENYEWE. Bahati mbaya serikali imetokea kuwaamini watu hao ambao ndio wanaoihujumu nchi hii na hakuna hatua zozote za kinidhamu zinazochukuliwa dhidi yao. Dawa ya watu hao ni kuwanyima ushirikiano sehemu za kazi na kuwaripoti kwenye vyombo vinavyohusika (hasa kwenye mitandao ya kijamii). Ni PM ili tuongee vizuri kuhusu UOZO huo.
 
Naunga mkono 100% maneno yako hawa wakuu wa shule ni wahujumu wakubwa wa kada ya elimu.Wanageuza ofisi za serikali kama taasisi zao.Wametawaliwa na rushwa pamoja na kutumia ofisi kwa maslahi yao binafsi.Wanawageuza walimu kama mitaji yao kwa kuwaomba rushwa ili wawape upendeleo maalum.UPUUZI HUU KWA NINI UNAACHIWA KTK NCHI YENYE KUFATA UTAWALA BORA?JE HAWA WATUMISHI WALIOJAWA DHAMBI YA RUSHWA NA MATUMIZI MABAYA YA OFISI WANAITAKIA MEMA ELIMU YA TANZANIA?
 
Idara ya elimu sekondari
Bagamoyo ina kila uozo wa rushwa katika maeneo mbalimbali. Rushwa hizo
zimejidhihirisha katika maeneo yafuatayo: 1.Kupangiwa kituo cha
kazi: Ili mwalimu apangiwe katika eneo zuri la kazi analazimika kutoa
chochote kwa Afisa mhusika.Kwa walimu wa kike wanalazimika mpaka kutoa
rushwa ya ngono.Utaona shule moja ya mjini ina walimu wengi wa kike.Wale
wasiokuwa na chochote hupangiwa vijijini.Wakati mwingine walimu hutumia
ndugu zao wakubwa ili wapangiwe mjini. 2.Mishahara hewa:Kuna
baadhi ya walimu watoro hata miezi sita wanapata mishahara wakiwa
hawafiki kazini.Wanatoa rushwa kwa wakuu wa shule na Afisa Elimu
sekondari ili wawalinde.Walimu hawa wamekuwa wakilipwa mishahara wasiyo
ifanyia kazi.Wengine wameajiriwa kabisa katika shule za private huku
wakiacha kabisa kufanya kazi katika shule zao walizoapangiwa na
serikali.Hali hii imekuwa ikidhorotesha elimu kwa kiasi kikubwa.
3.Kupata ruhusa ya kwenda masomoni.Ili mwalimu apate ruhusa ya kwenda
masomoni wakati mwingine analazimika kutoa rushwa ili apate
ruhusa.Walimu wasiotoa rushwa wananyimwa ruhusa kwa sababu mbalimbali.
4.Kupanda kwa madaraja. Kuna baadhi ya walimu
wana miaka mingi bila ya kupandishwa madaraja.Ili mwalimu apandishwe
daraja kwa wakati analazimika kutoa rushwa.Hata upandishaji wa madaraja
ni rushwa tupu na kujuana. 5.Fursa mbalimbali ktk ualimu
(Kwenda semina,kwenda kusahihisha mitihani ya kitaifa na kusimamia
mitihani ya kitaifa f2,f4 na f6.Hapa ndo kuna uvundo wa hali ya
juu.Rushwa na kujuana kuko nje nje.Kuna walimu wamejenga uswahiba na
urafiki wa hali ya juu na mabosi wa idara ya elimu sekondari.Walimu hawa
wanapewa fursa mbalimbali kwa kuwa wametoa rushwa au wanafahamiana na
mabosi wa idara ya elimu.Unakuta mwalimu mmoja kwenye kusimamia mtihani
wa f2 yumo,mtihani wa f4 yumo na mtihani wa f6 yumo kwa kuwa ametoa
rushwa au anafahamiana na Afisa Elimu au na mtendaji katika ofisi ya
elimu.Mwalimu huyo huyo kila mwaka hakosi kwenda kusimamia mitihani ya
kitaifa wakati kuna walimu wanasifa kama zake lakini hawateuliwi kwenda
kusimamia ati kwa kuwa wamegoma kutoa rushwa kwa wakuu wa shule au kwa
Afisa elimu na wasaidizi wake.Hali hii imepelekea kwa baadhi ya walimu
kuvunjika moyo wa kufundisha na baadhi yao wamesikika wakisema watahama
katika vituo vyao vya kazi au kuasi kwa kutofanya kazi kabisa.Uozo huu
wa ubaguzi,rushwa na kujuana umedhihirika katika shule karibuni zote za
Bagamoyo.Shule zilizokubuhu na uozo huu wa rushwa na kujuana katika kazi
maalum ni shule ya sekondari Kingani,shule ya sekondari Matimbwa,shule
ya sekondari Kiromo,shule ya sekondari Dunda,shule ya sekondari
Bwawani,shule ya sekondari Bagamoyo na shule ya sekondari Zinga. Mfano
kuna mtumishi mmoja katika idara ya elimu sekondari amekithiri kwa
vitendo hivi vya rushwa,baadhi ya walimu wa kike wamekuwa wakimpa rushwa
ya ngono ili awapange katika kazi maalum kama kusimamia mitihani.Hali
hii ikiachiliwa iendelee walimu wanaonyimwa fursa katika kazi maalum
wanaweza wakaleta athari kubwa kama kufanya kazi chini ya kiwango na
kuleta migogoro kazini.Hata hivyo sheria za kazi zinapinga matabaka na
ubaguzi mahali pa kazi.PCCB mmelala?

Afisa Elimu wa Bagamoyo ni Mwanamke na amehamia mwezi wa 7 mwaka 2013? Tuhuma za rushwa ya ngono zinamhusu yeye au? Ni vizuri kuwa specific hata kutaja majina ya wahusika ili wafuatiliaji wajue kwa kuanzia
 
Yeye DEO kwenye rushwa ya ngono hahusiki,ila kuna watendaji wa kiume katika ofisi yake wanapenda sana rushwa ya ngono.Ushahidi upo kuna huyu jamaa jina lake linaanzia na Chi anaomba sana rushwa ya ngono,kuna mwalimu mmoja wa kike ni mtu wake.Anafundisha shule moja ya sekondari ya kata ipo mjini kata ya mh.Waziri Kawambwa,basi huyu mwalimu anapewa upendeleo wa hali ya juu.Kila mwaka anapewa upendeleo ktk kazi maalum kama kusimamia mitihani mbalimbali ya kitaifa yaani f2,f4 na f6 huku walimu wengine wakiachwa,huyu jamaa ana kashfa kuomba rushwa ya ngono kwa walimu wa kike ili awape favour mbalimbali.Vilevile walimu wa kiume wanalazimika kumpa rushwa ili awapange kufanya kazi maalum.Ushahidi upo,unakuta mwalimu yupo masomoni lkn wakati wa mitihani anatoroka chuo na kutoa rushwa kwa Chi apangiwe kusimamia huku walimu ambao wako kazini kila siku wananyimwa fursa hiyo.Hali hii imejitokeza hata kwa walimu watoro wanaolindwa na huyu jamaa na kupangiwa kusimamia mitihani.
 
Back
Top Bottom