Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,115
- 2,771
Kwa wakazi wa Dar-es-Salaam masikini na tajiri, kwa muda mrefu , wamekuwa wakienda kwenye visiwa vya Mbudya na Bongoyo kwa ajili ya mapumziko ya masaa. Wanafunzi wengi sana kutoka kwenye vyuo wamekuwa wakimiminika kwa wingi siku za weekend kwa ajili ya mapumziko.
Gharama zilikuwa nzuri sana na Rafiki. Tsh. 3000 ndio kiwango ambacho watanzania wamekuwa wakitozwa. Ghafla gharama imeongezeka mara 4 (Tsh. 12,000). Kwa sasa Mtanzania yeyote kwenda Mbudya au Bongoyo ni mtihani. Wageni ndio kabisaaa Tsh. 40,000
Matokeo ya hizi gharama imekuwa mbaya sana. Wikendi iliyopita nilienda Mbudya na mdogo wangu, tukajikuta tuko watu 14. Kipindi cha nyuma kwa siku lile eneo, asubuhi hadi jioni hapakosekani watu 700 hadi 1000. Boti ilikuwa zinakuja na watu wengi sana, na pia kuwarudisha wengi. Kwa sasa, boti zinakuwa na trip moja au mbili
Kwa akili yangu hii ni Serikali kujihujumu yenyewe. Inapandisha gharama mara 4 na kujikosesha mapato ambayo yalikuwa ni ya uhakika. Wanafunzi wanategemea wazazi na boom ya chuo, hawawezi kujilipia hizi gharama kubwa. Mmachinga anayetaka kupumzika hata kwa siku moja, hawzi kumudu gharama.
Kwa mfano, Boti kwenda mbudya ni 10,000. Chakula 15,000 na Kiingilio ni Tsh. 12,000 jumla unalipa tsh. 37,000 au tuseme 40,000. Kwa watu hali ya chini, hii kodi ya chumba kwa mwezi. Na ndio maana Mbudya pamekauka. Wakushanya kiingilio wanalia sana, wanaomba watu wenye nguvu wafikishe hii kilio kwa wakubwa maana wanaumia sana