Idara ya uenezi CHADEMA ni kama imekufa, embu fanyeni bIdii kidogo

Idara ya uenezi CHADEMA ni kama imekufa, embu fanyeni bIdii kidogo

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
478
Reaction score
1,025
Katika watu makini katika wakati huu ni watu waliotengeneza hii slogan ya No Reform, No Election,.mmeweza. Wenzenu wanasema kazi na utu, wakati hizo kazi hazionekani Wala huo utu haonekani. No Reform, No Election ni kauli iliyobeba common course and unified ideology ndo maana tunaona ikiungwa mkono na wengi na kutetemesha wengine mpaka wanapoteana majukwaani.

Kikubwa Chadema mnapaswa kutrend, endeleeni kuwaelimisha wananchi wafikieni kwa namna yoyote Ile maana kwenye siasa mtaji ni watu na Chadema mara zote imekuwa ikipendwa na watu kwaiyo hicho kipengele mmekivuka.

Idara ya uenezi kweli nashindwa kuilewa maana sioni kazi kubwa ya kitengo hichi, zaidi naona mtu mmoja mmoja kwa nafasi yake aki push agenda, namuona Lissu akipambana kama mwenyekiti wa chama, namuona Heche naye akipigana kama makamu mwenyekiti wa chama, tunamuona karibu mkuu naye hivyohivyo ila hatuoni idara ya uenezi ikitake charge, naomba mliweke hili vizuri Ili mapambano yaende kwa nguvu moja.

Pia tunaomba kuelewe vizuri mfumo wa mapambano kama ulivyoamualiwa ni no Reform No Election, sasa tunafanye?

Tunazuia vipi uchaguzi kufanyika? Ni kutoshiriki uchaguzi? maana Chadema isiposhiriki uchaguzi, vyama vingine vitashiriki na hiyo haiharamishi uchaguzi kwaiyo mwisho wa siku uchaguzi itafanyika na Rais atapatikana.

Je reform zinazotakiwa kufanyika zinaweza kufanyika kwa huu muda uliobaki? Je kama ni reform zinazoweza kufanyika na kwa makusudi zinakwamishwa na watu baadhi, kwanini Chadema msifungue mashtaka mahakamani kushirikiza hizo reform maana mwisho wa siku lazima uchaguzi ufanyike na Rais tumpate.

Chadema naomba mtoe mwongozo kwa wananchi Ili wajue mwelekeo na mipango mbadala pale mambo yatakapokwenda tofauti na matarajio. Kikubwa tu tusikubali kuweka rehani amani ya nchi yetu kwa maslahi ya kisiasa. Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania.
 
Subiri waje kuilaumu CCM ndio sababu idara yao imefeli.
Tunawakumbusha mapema, haya mapambano siyo mepesi, Makala anapigwa chini, wakija watu kama kina Polepole wanaojua kujenga hoja na kupangua hoja watatafutana.. kikubwa mapambano yanahitaji maandalizi na strategy
 
Polepole ndio mwepesi sana wa kukimbilia mbeleko bora hata mumuache huyu Makalla aliyechanganyikiwa.
 
bint rupia huyo anatakiwa kuchangamka

Kweli ,nimeona Hadi mikutano Yao sauti zinaingiliana sana sana sijui wanakwama wapi
 
Tunawakumbusha mapema, haya mapambano siyo mepesi, Makala anapigwa chini, wakija watu kama kina Polepole wanaojua kujenga hoja na kupangua hoja watatafutana.. kikubwa mapambano yanahitaji maandalizi na strategy
Nikwambie tu kwamba hili No reforms No election limevimbia pa baya hata aje nani. Anza kutaka kura yako iheshimiwe kwa kusimamiwa na Tume isiyowekwa na mgombea wa CCM,kataa kutekwa wakati polisi wa usalama wa raia na mali zao wanalipwa kodi yako,Pendekeza umuhimu wa kuwa na Tume inayoweza kushitakiwa ikikosea, Tamani kuona watawala kama wanapokea matakwa ya wananchi kwa kuwa mamlaka yanatoka kwa wananchi.
 
Muongozo tunatoaje wakati na sisi tumechaganyikiwa
Inatakiwa kuzuia matamko ya kila mwanachama, lazima idara ya uenezi ndo ihusike na matamko yote yanayohusu misimamo ya chama
 
Chadema haina nguvu yoyote kwasasa,hawana hoja inayogusa maisha ya watanzania,hawana hata fununu ya rushwa serkalini!!
No lifomu no elesheni wananchi hawaelewi icho kiinglish they are just wasting their time!!!
Wataaibishwa na mama mpaka washangaeee🤣🤣
 
Chadema haina nguvu yoyote kwasasa,hawana hoja inayogusa maisha ya watanzania,hawana hata fununu ya rushwa serkalini!!
No lifomu no elesheni wananchi hawaelewi icho kiinglish they are just wasting their time!!!
Wataaibishwa na mama mpaka washangaeee🤣🤣
Siyo kweli
 
Back
Top Bottom