Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Mdau wa JamiiForums.com anasema kila kunapotokea Janga hasa la Moto taarifa pekee inayotoka ni Moto kuzimwa ukiwa umeteketeza kila kitu au kubakiza sehemu ndogo sana.
Anatolea mfano kuungua kwa Shule, Masoko, Mlima Kilimanjaro uliowaka kwa zaidi ya wiki 2 ambapo anahoji tatizo ni Idara kukosa utaalamu wa kudhibiti na kuokoa majanga, hakuna vifaa vya kisasa au hazichukulii kwa uzito majanga hayo?.
Anashauri Serikali iwekeze bajeti kubwa kwenye Idara za Uokoaji ikiwemo Zimamoto pamoja na kujenga Mabomba ya Kuzima Moto (Fire Hydrant's) kwenye mitaa na maeneo muhimu kama Hospitali, Masoko, Majengo ya Ibada, Shule n.k.