Idd Ninga: Je, wajua kambi ya wakimbizi na Kipoland iliyokuwa Tengeru?

Idd Ninga: Je, wajua kambi ya wakimbizi na Kipoland iliyokuwa Tengeru?

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
Sehemu ya kwanza.


Kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Tanzania ilikuwa ikujulikana kama Tanganyika.

Tanzania ni moja kati ya nchi kadhaa duniani zenye kuhifadhi wakimbizi na kundi kubwa ni la wakimbizi wanaokimbia vita katika nchi zao.

Licha hiyo,Tanzania iliwahi kuhifadhi wakimbizi wazungu ambao na wao walikimbia vita katika taifa lao kama wafanyavyo wakimbizi wa Congo au Rwanda.

Ni sehemu ya historia katika nchi yetu ambayo haijulikani na wengi na hata unapowasili katika eneo la Tengeru palipokuwa kambi hiyo si ajabu kukuta hata wakazi wa eneo hilo hawatambui kuwa kulikuwa na kambi kubwa ya wakimbizi.

Nilijaribu kufuatilia sana historia ya eneo hilo na kweli nilibahatika kumpata mzee mmoja ambae aliweza kufanya kazi enzi ya wapoland hao lakini nilipomueleza kuwa nafuatilia historia ya eneo hilo na jinsi wazungu hao walivyoishi,mzee huyo aligoma kuniambia chochote mpaka nitoe kitu kidogo kwani aliamini naitafuta historia hiyo kwa ajili ya biashara.

Zamani kabla ya ujio wa wakimbizi hao eneo hilo lilikuwa halijulikani wa jina Tengeru lakini baada ya wao kufika ndipo eneo hilo lilipata jina la Tengeru linalotokana na MTO TENGERU.

Ilikuwa ni safari ndefu yenye mateso ambayo iliwafikisha hapo katika eneo la Tengeru.

Mwaka 1942 hadi 1952 historia iliandikwa.

Je, ilikuwaje katika safari yao mpaka wakafika eneo la Tengeru?

Ungana nami katika sehemu inayofuata.

Maoni na maswali/ushauri=iddyallyninga@Gmail.com
 
Samahani, huwa natumia simu katika kuandika hivyo nachoka wakati mwingine kuandika.
Nitaendelea, ondoa shaka.
 
So kweli kuwa walikuwa wakimbizi Bali wale walikuwa mateka wa vita, siyo tengeru tu hata iringa pale ifunda walikuwepo wapoland hao.
 
Walikuwa mateka wa Vita.Pale Ifunda walikaa sana Ifunda Tech,ndio walikuwa walimu wa Ufundi mbalimbali pale Technical School.Wakaleta Post Office hata kabla ya miji kama Mafinga na Njombe hawajapata.Enzi hizo ilikuwa kuwa na Post Office ni jambo kubwa kubwa sana.

Ndio walikuja kujenga Kanisa Katoliki Ifunda kama sehemu zao za kazi za kila siku,waliipenda Ifunda na Tengeru sbb ya hali ya hewa.
 
Mateka wa Vita gani mkuu? Na inakuwaje mateka wa Vita wajenge na wafundishe shule Yani wawe huru namna hiyo?
Walikuwa mateka wa Vita.Pale Ifunda walikaa sana Ifunda Tech,ndio walikuwa walimu wa Ufundi mbalimbali pale Technical School.Wakaleta Post Office hata kabla ya miji kama Mafinga na Njombe hawajapata.Enzi hizo ilikuwa kuwa na Post Office ni jambo kubwa kubwa sana.

Ndio walikuja kujenga Kanisa Katoliki Ifunda kama sehemu zao za kazi za kila siku,waliipenda Ifunda na Tengeru sbb ya hali ya hewa.
 
Samahani,huwa natumia simu katika kuandika hivyo nachoka wakati mwingine kuandika.
Nitaendelea,ondoa shaka.
mzee alikuwa sahihi kujizuia kutoa taarifa mpaka umpe pesa, alijua information ambayo angekupa ungekuja kuitumia kwa interest zako binafsi na sio kuhabarisha umma.

kitendo cha kuleta story nusu ni dalili tosha ya kile alichokwambia yule mzee.
 





Sent from my N100 using JamiiForums mobile app

Asante Kiongozi!

Hapa inaonesha takribani wakimbizi elfu 20 toka Poland walikuja Afrika miaka ya mwanzo mwa 1940. Tanganyika ilikuwa na kambi 9, Kenya 5, Uganda 5, Afrika ya Kusini 3, Zimbabwe 3 na Zambia 2.

Kwenye hii video wanataja kambi 3 za Tanganyika. Kambi kubwa ilikuwa Tengeru Arusha, na ilikuwa na Wapoland takribani 5,000 (kambi kubwa kwa Afrika), Kambi nyingine iliyotajwa hapa ilikuwa Kidugala Njombe ambayo ilikuwa na Wapoland kama 1,100 na nyingine ilikuwa Kondoa Irangi, ambayo ilikuwa ina wapoland kama 500. Articles nyingine zinataja makazi yasiyo ya kudumu yalikuwapo Ifunda, Morogoro, Kigoma, Dar es Salaam, Iringa na Tosamaganga.

Wanasema Wapoland wachache sana walibaki Afrika hadi kufikia mwaka 1950. Wengi walirudi Poland, na wengine walihamia Marekani, Canada, Argentina, Ufaransa, na Australia. Karibu wakimbizi wote waliondoka Afrika baada ya vita ya pili kuisha. Kambi ya Tengeru ilifungwa nusu ya pili ya mwaka 1952. Watu mamia wachache walibaki Tanganyika. Taarifa za mitandao zinasema mpolandi wa mwisho, Mr. Edward Wójtowicz, alizikwa Tengeru mwaka 2015.
Screenshot_20220119-064215_DuckDuckGo.png
Screenshot_20220119-064318_DuckDuckGo.png
Screenshot_20220119-064302_DuckDuckGo.png

Screenshot_20220119-062935_DuckDuckGo.png
 
So kweli kuwa walikuwa wakimbizi Bali wale walikuwa mateka wa vita, siyo tengeru tu hata iringa pale ifunda walikuwepo wapoland hao.
.... it makes sense; ndio maana maeneo ya kuanzia baada ya Ipogolo hadi mbele kidogo ya Ifunda naonaga makanisa ya ki-Orthodox sipati majibu. Kumbe ni matokeo ya historia. Walitekwa na nani? Na ikawaje watoke kote huko Poland hadi Ifunda?

Idd Ninga malizia hii stori yako ulitoainzisha 8 yrs ago tafadhali.
 
Hawa wakimbizi kutoka Poland waliotokana na vita ya pili ya dunia. Waliweka kambi yao maeneo kadhaa Tanzania ikiwemo Tengeru, Kidugala, Kondoa, Ifunda, Kigoma, Dar, Tosamaganga na Kiabakari.

Kambi ya Tengeru ndiyo iliyokua kubwa kuliko zote, ilikua na nyumba 947 na wakazi 4018.

Pale Tengeru walianya maendeleo ya Kilimo na kujenga shule kubwa ambayo kwa sasa ni Chuo cha Maendeleo ya Jamii.

Eneo la Tengeru kuna makaburi zaidi ya 140 ya wapolish waliofariki kati ya mwaka 1942-1952 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa influenza na magonjwa mengine ya kuhara.

Baada ya vita ya pili ya dunia, wakimbizi hawa walianza kurudishwa Ulaya na kuamriwa ibaki kambi moja tu Tanganyika ambayo ni Tengeru.

Mpoland wa mwisho kuzikwa makaburi ya Tengeru ilikuwa mwaka 2015, aliitwa Edward Wojtowicz.

Eneo hilo la makaburi limezungushiwa ukuta miaka ya karibuni kutokana na baadhi ya watu kwenda kuyafukua wakiamini kuna vito vya thamani.

Kila tarehe 1 Novemba wafanyakazi wa ubalozi wa Poland Tanzania hukusanyika eneo hili kwaajili ya kumbukumbu.
 
Kuna wengine walifariki walizikwa bongo
Hat ukienda makaburi ya kinondoni pale
Ukingia utakutana na taarifa zao kwenye bongo
Lao

Ova
 
.... it makes sense; ndio maana maeneo ya kuanzia baada ya Ipogolo hadi mbele kidogo ya Ifunda naonaga makanisa ya ki-Orthodox sipati majibu. Kumbe ni matokeo ya historia. Walitekwa na nani? Na ikawaje watoke kote huko Poland hadi Ifunda?

Idd Ninga malizia hii stori yako ulitoainzisha 8 yrs ago tafadhali.
Nitarudi Tena kuandika zaidi pamoja na kuleta picha zaidi
 
Nitarudi Tena kuandika zaidi pamoja na kuleta picha zaidi
... miaka 8 umri wa mtu bro! Ni wangapi walitamani kuipata stori yote lakini wameondoka bila kuipata; ndani ya miaka 8 tumepoteza wapendwa wengi mno. Utarudi baada ya miaka mingapi kaka?
 
Back
Top Bottom