Natania
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 262
- 217
Heshima kwa waungwana wote. Nimeamua kujenga ka-jumba kangu Morogoro na ningependa kujenga kwa matofali ya kuchoma. Swali - Je Kuna mtu anajua tofali imara za kuchoma zinapatikaneje (kwa Morogoro)? Je nawezakuzitengeneza mimi mwenyewe hizo tofali ama mpaka ninunue kwa wataalamu waliobobea? Kwa bahati mbaya tofali hizi nimeishia kuona kwenye picha (mojawapo ni hiyo niliyoatach pamoja na kwamba tofali zake hazing'ai) ama wakati napita sehemu mbalimbali. Aina ya tofali ninayovutiwa nayo ni ile yenye mng'ao (nadhani hupigwa polish kuongezea mng'ao na nyumba ikijengwa kwa tofali kama hizo huwa haipigwi lipu). Mara nyingi tofali hizi huwa zinatengenezwa kwa size ndogo sana (tofauti na tofali za kuchoma zinazotengenezwa kienyeji hata vijijini ambazo ni kubwa kiasi).
View attachment 76712
Tafadhali funguka kama unadata (aina, bei, any relevant information)
View attachment 76712

Tafadhali funguka kama unadata (aina, bei, any relevant information)