IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

Sasa hapa umeongea point mkuu.Mada hii ni ubora wa jeshi husika kwenye uwanja wa mapambano.Ndio maana nikaleta hii mada toka mwanzo
 
Karibu uchangie na nimeyapokea maoni yako.Asante kwa ushauri
 
Nyamizi,
Sina chochote binafsi na yeyote hapa JF.

Wala sijuani na yeyote hapa JF.
Wala sijatunisha msuli.

Nguvu yangu ipo katika kalamu yangu.
Wewe ndiyo umeniandikia kuhusu Nelson na nimekujibu.
Mzee said mohamed,mdogo wako nipo na sio busara ukabishana na wengine tuendelee na mada yetu.Kutofautiana hoja au mitazamo sio hoja.Ukweli utabaki kua wewe ni kaka mkubwa na mimi ni mdogo wako.Kuna maisha nje ya jamii forum
 
Karibu tuendelee kaka yangu na uwe na moyo wa kiume wa kupokea hoja pinzani na sio unakua emotional kihisia na kiroho kama watotoNina mada ya CCM pia kama chama bora na pendwa Afrika na dunia mzima.Karibu na kule uchangie mzee wangu
 
Mimi sio mbishi au naharibu mada ila angalizo langu tangu mwanzo lilikua tusichangie kisiasa au kidini au kiitikadi.Bali tuchangie kama wachambuzi wa mambo ya kijeshi.Na ndio hiyo ilikua tofauti yangu kuu na kakangu na jirani yangu pia mzee said mohamed
 
Karibu mchangie kijasusi na kiubora wa majeshi husika katika uwanja wa mapambano.Mkijadili kidini mtakwama na mtaishia kila mmoja kuvutia upande wake.Karibuni mchangie kama nilivyoleta mada.Na leo nitamjadili kachero namba 448 ambae picha yake moja ilipatikana enzi hizo akiwa jeshini.Lakini baadae alifanyiwa operasheni ya kumbadili sura mara kadhaa kuficha uhalisia wake na ubora wake kama mkufunzi wa majasusi wa IDF na nchi nyingine washirika
 
IDF amefanya military missions nyingi kuzidi USArmy!? Kuliko RAF!?
Na hizo military missions alizofanya ni za aina gani!? Rescue missions, peacekeeping missions, humanitarian military missions, military raids, military invasions au etc!? Na je wamefanikiwa vipi kwenye hizo mission zote. Success rate!?


Hapo kwenye hiyo list hizo mission nyingi za israel tuoneshe ziko wapi au labda kama una reference yako mbadala inayoonesha list ya military ops za IDF kuzidi mataifa mengine yote utupe.

Na tangu lini ubora wa jeshi ukapimwa kwa military missions!? Hii ni crietria mpya bila shaka lakini hata hvyo haimake sense. Mfano TPDf utasema ni jeshi bora kuliko Egypt kisa tu Tpdf wamehusika kwenye misheni nyingi kuliko!? Unataka kusema US ni dhaifu mbele ya TZ kwa sababu US alifeli owenye mission yake ya cuba (bay of pigs) wakati TZ walifaulu huko Comoro. Unaweza ukawa na utitiri wa misheni na bado ukawa mchovu tu.

Kwa mujibu wa global firepower ubora wa jeshi huzingatia vigezo muhimu zaidi ya 60
  • Man power; popln, available manpower, fit for service, active personnel, active reserve, paramilitary, etc
  • Equipments & technology; aircraft fleet strength, tank strength, naval fleet strength
  • finaces; defence budget, xternal debt, ppp etc.
  • logistics; airports, ports, etc
  • Resources
  • location

IDF ni moja ya majeshi bora lakini kusema ni bora zaidi duniani ni uongo wa mchana kweupe. Tusisahau pia mchango wa marekani na washirika wake kwenye jeshi la Israel

Mossad wamefanya ops zaidi ya elf moja duniani!? Kiko wapi chanzo cha hii taarifa!? Au mtu ukijiskia tu unaandika namba yeyote unayoitaka!? Yaani operation moja, mbili, tatu, ...kumi, ...mia moja mpaka elfu moja na zaidi. Duh! Huu pia ni uongo. Operation za mashirika ya kijasusi huwa ni siri (classified). Inakuwaje wewe uwe unazijua zote elf moja na zaidi!? Wewe ni Mossad!? Hata afisa wa Mossad mwenyewe hawezi kujua ops zote zinazofanywa na shirika lake maana nyingi zinafanywa kwa basis ya 'need to know' yaani unajua kile unachopaswa kujua. Labda kama wewe ni mossad mwenye highest level of clearence. Labda! Hii JF bwana kila mtu anaweza kuwa kila mtu.

NB: Hakuna namna yoyote unaweza kupima ubora wa shirika la kijasusi objectively.
 
Upo sahii kwa maoni yako kaka na maswali yako ni ya msingi kabisa.Lakini mada inazungumzia ubora wa IDF katika uwanja wa mapambano na ubora wa Mossad katika operasheni zake akiwa washirika zake kama nilivyoletea mada.Nitakujibu baadae baadhi ya maswali yako.Lakini kwa sasa nitajadili zaidi kumuhusu kachero 448 wa Mossad.Karibu sana ndugu yangu triga
 
Kumzungumzia kachero 448 hakuipi uzito mada yako kuhusu IDF kua jeshi bora zaidi duniani. Bado haujaitendea haki mada yako.

Ningependa kuona ukizungumzia vigezo ulivyotumia kuwarank IDF kama jeshi bora zaidi duniani. Tupatie na references ili tujiridhishe na tujifunze zaidi.

Huko unakoelekea sasa hivi, unatutoa nje ya mada!
 
Usiwe na haraka mkuu tunaendelea.Lakini kuna wadau wameniomba tumjadili kachero 448 afu tutaendelea.Mada inaendelea kua na amani
 
Kwani waislamu ndio wavaa kobaz?
 
Kwani waislamu ndio wavaa kobaz?
Tadic,
Tuchukulie kuwa hakuwakusudia Waislam ila wengine.

Hili litakuwa jambo jema.

Au tuchukulie wewe ni mgeni wa kejeli hizi.

Itakuwa bora zaidi.

Waingereza wana msemo: "Ignorance is bliss."
 
Wa
Tadic,
Tuchukulie kuwa hakuwakusudia Waislam ila wengine.

Hili litakuwa jambo jema.

Au tuchukulie wewe ni mgeni wa kejeli hizi.

Itakuwa bora zaidi.

Waingereza wana msemo: "Ignorance is bliss."
Wavaa kobazi sio kejeli mzee wangu bali ni utambulisho.Sawa na mapadri kuvaa magauni ya kiume mzee wangu
 
Karibu mjadala kaka ila mada tunazungumzia ubora kwenye uwanja wa mapambano
Wamepambana na Nani?? Hizbola na Hamas??? Apigane vita Ile ya Mano O Mano na nchi ilisimama vizuri. Achana na story za propaganda za kuwa fanya wao ni noma. Wamekaa hapo kwa kujifanya wamefuata bibble. If so mbona hawachukuo ardhi ya LEBANON maana wakipewa yote....according to Bible. Hawawezi sababu wanajua the effect ya vita ya nchi iliyojitosheleza. Utashinda but utapigika na wewe. Mara Mia sisi tuna record ya kumpiga NDULI.
 
Karibu uchangie ila usiwe na mihemuko mkuu
 
Kwa mara ya pili IDF wamefanyiwa surprise attack na HAMAS ile inayofanana na hali walizokutana nazo kule Beirut LEBANON na JORDAN miaka ile ya 60,s na 70,s na 80,s kipindi cha maazimio ya waarabu kuifuta kabisa Israel kwenye ramani ya dunia na kukataa historia ya wayahudi kama watu huru bali vijakazi na watumwa wa waarabu.Ila kihuasilia haiondoi ubora wao katika nyanja za kivita.Nakumbuka wakati wa vita vya YOMM KIPPUR wiki ya kwanza kila mtu alijua IDF wameshindwa na majeshi ya EGYPT waliua na kuteka zaidi ya wanajeshi 700.Na kule GOLAN HEIGHTS majeshi ya makomando ya SYRIAN ARMED FORCES yaliiteka tena upya milima ya GOLAN na kuweza kuchukua mateka wanajeshi 200 na zaidi wa IDF.
Lakini kilichotokea wiki zilizofuata ni simulizi ambayo kila mchambuzi wa historia za kijeshi anazifananisha na jinsi WAAJEMI walivyoweza kuyazuia majeshi ya OTTOMAN EMPIRE kuvamia aridhi yao ya UAJEMI KARNE ILE.
Kiufupi IDF ilifeli suala zima la kiitelenjensia kuzuia suprise attack za Hamas militant kama ilivyofeli kuzuia suprise attacks za EGYPT NA SYRIA kwenye YOMM KIPPUR WAR.
Lakini hilo halitoi ubora wa intelenjisia ya IDF na MOSSAD na washirika wao kote duniani.
Tusubiri matokeo je Hamas na Hezbollah na kamati kuu ya Mahayatolah wa serikali ya mapinduzi ya kiislamu ya IRAN kama watafanikisha malengo yao yenye mtazamo wa kidini unaosema kua WAYAHUDI NI MAADUI WA WAISLAMU NA WAARABU NA HADHI YAO PEKEE NI KUA VIJAKAZI NA WATUMWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…