Msemaji wa Jeshi la Israel Brig. Gen. Daniel Hagari kupitia vyombo vya habari amewatangazia wananchi wa Israel kuwa mashambulizi ya Iran yaliyoelekezwa katika mji wa Tel Aviv yamekwisha hivyo watoke kwenye maficho yao waendelee na shughuli zao ila kwa tahadhari.
Brig. Gen. Hagari amekiri kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ni makali yaliyohusisha makombora zaidi ya 180 ila anasema hawana taarifa za vifo wala majeruhi kwakuwa makombora mengi yalinaswa na mifumo ya ulinzi wa anga na pia kufuatia taarifa za kiintelijensia zilizotolewa awali, baada ya king'ora kulia, wananchi wote waliingia kwenye vyumba vya kujikinga na mabomu (bomb shelter) hivyo wanaamini wako salama.
Hata hivyo, Brig. Gen. Hagari kasisitiza kuwa, Iran itajibiwa kwa siku na muda Israel itakapochagua, Israel imejiandaa vya kutosha.
View: https://youtu.be/r9HupxV5IOs?si=jHUV3plr3b93ZfJ5
PIA SOMA
- Iran yarusha Makombora takriban 200 kuelekea Israel, Rais Biden aagiza Jeshi la Marekani kuyazuia