Ukweli ni kwamba hizi chokochoko za Tanzania dhidi ya Kenya zikiendelea hivi, ni wazi hatutaishia pazuri, siungi mkono sera za kuwafurusha Watanzania walioko huku, pia sikubaliani na kauli za kugomea bidhaa kutoka Tanzania, lakini namkubali Duale kwa hili la kuhimiza Tanzania ijadiliwe bungeni, uhusiano wetu naa nyie umeharibika pakubwa, tunadanganyana kwa kukenua meno, lakini kiukweli nyuma ya pazia kuna mengi yanatokota.
Muda umefika hili lijadiliwe na kila kitu kiwekwe juu ya meza, ieleweke wapi tunakwenda. Hata kwenye ndoa, ipo wakati wana ndoa huamua kutibua ili liongelewe. Wabunge wetu waibue mada ya kujadili uhusiano wetu na Tanzania maana serikali yetu imegoma kutulinda dhidi ya udhalimu wenu.