Idris Sultan afikishwa katika Mahakama ya Kisutu. Ashtakiwa kwa kumiliki laini ya simu isiyo na jina lake. Aachiwa kwa dhamana

Kwani alipost kwa nia ya kukuchekesha au kajipostia zake tu.
Mimi nampenda sana Idris ana akili sana na hua ananichekesha na kunifunza mambo kutoka kwenye post zake
Kwa vile wewe ni Mrs Van sishangai lakini mimi binafsi naungana na wadanganyika wengi ambao bwana yule hatuchekeshi lolote tunao comedians kama kina Joti et al
 
Bongo nyoso nyoso,yani Mr blue aliona neno figisu figisu Kama halitoshi kuwaelezea wabongo jinsi walivyo na zengwe
 
Adhabu kutokana na kifungu gani Cha Sheria ?
Kumbe na wewe unapenda kuzichekea picha za watu...!
Kwanini usiichekee picha yako ?
Kasome Sheria ya Mtandao ya Bullying.

Wasanii mjiheshimu basi, acheni kujichekesha chekesha kwenye picha za watu kama dishi limeyumba vile, haina faida kwa Jamii inayo wafuatilia.
 
Kweli ile suti ova size,nakazia ile suti ni single piece in tanzania fundi alieshona alikua kipofu
Ule ulikuwa mtindo wa zama zile, tatizo mmezaliwa juzi juzi hapa.
Unazijua Suruali za Mtindo wa Kamanyola ?
Au Pekoz.
Kama mnashindwa kuelewa Ulizeni Wahenga.
Kulikuwa na Makoti yanavuka Magoti.

Wacheni Utoto Basi.
 
Magufuli anajikuta immortal ahahahaha!
Na ninavyojua kucheka watu ingekuwa mimi nacheka hadi naanguka chini
Kimsingi ile picha wanae na wajukuuu wanaicheka. Na wala sio ajabu wengi wetu hua tukiona picha za zamani za wazazi wetu hua tuna cheka.

Ina julikana wazi picha za wakati woa au hata mavazi ya wakati wao ni tofauti na sasaaa.

Hivi Kuna ambae ameshawahi kuadhibiwa kwa kuicheka picha ya zamani ya wazazi wake. ? .huuu utukufu wanao jaribu kumpa hana na hatakua nao hadi kifo chake . piriod

Sent from my SM-A500F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani ushauri wako umepuuzwaa, hata wao wameona aibu kufungua mashitaka ya kijinga kiasi hicho ulicho fikiria.

Sent from my SM-A500F using JamiiForums mobile app
 
Kosa ni la Mkuu wa nchi. Kwanini avae mavazi ya kuchekesha namna ile? Kuna tatizo hapo.
 
Wamefanya sawa kuliko kuweka ile picha maana ingesambaa dunia nzima.

Watu tunajiogopa hata tukipiga picha tunajishangaa, kila umri unakuwa na mambo yake.

By the way, mwambieni huyo dogo asipende utani na watu wakubwa, Siyo wote wana vifua vya utani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23]mwanzo kucheka picha,
Sasa kumiliki laini isiyo na jina lake..
[emoji23][emoji23]
TZ haiishiwi kwa vituko
 
Hapana amehurumiwa tu, alikuwa anaenda, Mzee akasema Mwacheni anatafuta Kiki tu
Hiyo Kiki ameitoa mwenyewe huyo mzee. Angepuuza tangia mwanzo kingepungua nini kwenye huo uzee wake. ?

Ajikite kwenye mambo makubwa ya ki nchi na sio hivi vituko vya kitotoo. Mzee mzima kuhangaishwa na vicheko vya kitotoo ni upuuzi ulio pitiliza .

Siku akichorwa hivi kama trump si atapiga watu risasi hadharani. Teheteheee tehetehee

Sent from my SM-A500F using JamiiForums mobile app
 

Hahahaaaa!

Magu na wala vumbi hawawezi kuelewa hata kidogo.

Jamii yenye idadi kubwa ya watu wenye negative IQ ni ya kuonewa huruma tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…