Idris Sultan amuonya Billnass yasimkute matatizo kama ambavyo yalimkuta yeye kuitwa kituo cha Polisi

Idris Sultan amuonya Billnass yasimkute matatizo kama ambavyo yalimkuta yeye kuitwa kituo cha Polisi

Dunia yakoo

Senior Member
Joined
Nov 23, 2019
Posts
139
Reaction score
214
IDRIS AMPA 'ONYO' BILLNAS

Mchekeshaji na Muigizaji Idris Sultan amesema rapa Billanass amuombe sana Mungu yasimkute matatizo kama ambavyo yalimkuta yeye ya kuitwa Kituo cha Polisi maana atapata tabu sana.

Idris Sultan amefunguka hayo mara baada ya Billnass kumletea utani Baada ya kuwekwa ndani kwa siku kadhaa kwa kosa la kutumia Kompyuta kwa kuichapisha picha yake na Rais Magufuli. Billnas aliandika "Nipeni Taarifa za Ndugu Yangu, kalala kituo gani ?? Au Kalala na Nani??" huku akiambatanisha na Picha ya Idris

"Watu walihitaji kufurahi na wanahaki ya kufurahi, naamini hata Billnass hana nia mbaya na mimi sidhani kama amefurahia kweli ila anajua haya mambo yanatokea na yatakwisha, vyote kwa vyote ni utani tu na mtu yeyote anaweza akafanyiwa na hata nikishikiliwa tena sitegemei watu walie au wahuzunike" amesema Idris Sultan
 
Sasa hivi anaendaga sentro kuuza chai na vitumbua usubuhi.
 
Watanzania wanaishibkwa woga sasa, hata kutaniana ni kwa woga.
 
Au wajeda wamepitisha ngozi ngumu kwenye Linda box La jamaa
 
[emoji1787][emoji1787] ndani si kuzuri
 
Back
Top Bottom