Mshindi wa big brother mwaka 2014 idris sultan tetesi zilizozagaa mitandaoni kwamba kuna mtu alimpa pesa zake kwa ajili ya lakini alizitumia kinyume na makubaliano.
View attachment 343854Ikumbukwe mshindi huyo wa Big Brother Africa
2014, alipata zaidi ya milioni 500. Pesa ambayo
alidai aliitumia kuwekeza katika biashara
mbalimbali, na baadae aliweka wazi kwamba
pesa hizo zilishaisha.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Idris
amesema ni kweli kuna mtu alikuwa anafanye
naye biashara lakini akamwingiza mkenge.
“Kuna watu ambao nimeweza kufanya nao kazi,
lakini wakaaribu baadhi ya mambo, nisingependa
kuliongelea kwa sababu kuna baadhi ya vitu
ambavyo wameviharibu sana, na hawakuweza
kuviweka sawa,” alisema Idris.
Aliongeza, “Yaani kama kupunyua, hivi vitu
vinatokeaga katika sehemu yoyote, kwenye
kampuni, kwenye nini. Kuna watu wanaweza
wakafuja mali zako au wakafanya vitu vibaya
kinyume na mlivyo kubaliana. Kwa hiyo siyo
inshu kubwa sana kwangu, kwa sababu maisha
yanaendelea na milango inafunguka,”
Stori ambazo zilikuwa katika mitandao ya kijamii
zilikuwa zinadai kuwa meneja wa zamani wa
Idris, ndiye ambaye alimwingiza mkenge Idris,
kitu ambacho Idris hakupenda kukizungumzia
zaidi.
Pia Idris amesema kwa sasa amepata
menejimenti mpya ambayo itakuwa
inamwongoka katika kazi mbalimbali