Ana msingizia meneja wa zamani ili kuficha ukweli tu biashara kweli alifanya ila ya kununua mimba, mbona hakueleza kabla haja uziwa mimba tena ya mapacha na Tasa na akainadi sana tu, pengine mbuzi wa kwenye gunia asinge muona na hata wa kwenye fuko la plastic transparent pia haku muona? mapacha! kwa shokolana lile ubaki na kitu? aondoe ulimbukeni wake Pambaf.aseme tu wema kaitafuna na asisingizie biashara
na yule madam anajua sana kuedeal na kulea watoto,mtu kama diamond ngastuka mapema...Ana msingizia meneja wa zamani ili kuficha ukweli tu mbona hakueleza kabla haja uziwa mimba tena ya mapacha na Tansa,na akainadi sana tu pengine mbuzi wa kwenye gunia asinge muona na hata wa kwenye fuko la plastic transparent pia haku muona? mapacha! kwa shokolana lile ubaki na kitu? aondoe ulimbukeni wake Pambaf.
Sio WATU wametafuna aseme MTU ametafuna mbona maombolezo hayo hatuku yasikia kabla? Chezea MADAME,mchwa yule.Mshindi wa big brother mwaka 2014 idris sultan tetesi zilizozagaa mitandaoni kwamba kuna mtu alimpa pesa zake kwa ajili ya lakini alizitumia kinyume na makubaliano.
View attachment 343854Ikumbukwe mshindi huyo wa Big Brother Africa
2014, alipata zaidi ya milioni 500. Pesa ambayo
alidai aliitumia kuwekeza katika biashara
mbalimbali, na baadae aliweka wazi kwamba
pesa hizo zilishaisha.
Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Idris
amesema ni kweli kuna mtu alikuwa anafanye
naye biashara lakini akamwingiza mkenge.
“Kuna watu ambao nimeweza kufanya nao kazi,
lakini wakaaribu baadhi ya mambo, nisingependa
kuliongelea kwa sababu kuna baadhi ya vitu
ambavyo wameviharibu sana, na hawakuweza
kuviweka sawa,” alisema Idris.
Aliongeza, “Yaani kama kupunyua, hivi vitu
vinatokeaga katika sehemu yoyote, kwenye
kampuni, kwenye nini. Kuna watu wanaweza
wakafuja mali zako au wakafanya vitu vibaya
kinyume na mlivyo kubaliana. Kwa hiyo siyo
inshu kubwa sana kwangu, kwa sababu maisha
yanaendelea na milango inafunguka,”
Stori ambazo zilikuwa katika mitandao ya kijamii
zilikuwa zinadai kuwa meneja wa zamani wa
Idris, ndiye ambaye alimwingiza mkenge Idris,
kitu ambacho Idris hakupenda kukizungumzia
zaidi.
Pia Idris amesema kwa sasa amepata
menejimenti mpya ambayo itakuwa
inamwongoka katika kazi mbalimbali
What a nice comment!Pesa isiyokuwa kwenye mzunguko siyo pesa
Hahahahaha mimi binafsi nilishajua akibaki hapo hakatizi miaka mitatu atabaki hana kitu... Nilipochoka ni pale aliponunua ile nyumba kule Africana.. Nikajiwazia tu kwanini huyo dogo asingerudi Arusha akaanzia palepale kwao au akarent nyumba Njiro au Sakina.. Biashara ya madini kwa huo mtaji ingemlipa mno.. Mbaya zaidi nilivyosikia anakichafua na wema nikajua ndio habari yake imekwisha..
Hahahaha...bro umeeleza vizuri sana
Japo uliwahi kuniambia wewe hua hujadili watu humu sijui leo imekuaje mkuu
samahani lakini usinitukane mkuu nimewaza kwa sauti tuu...Kudos!
Nakumbuka baada ya kushinda hizo pesa, tulikuwa mahali na Dk. Ngowi, mchumi na bonge la entrepreneur akasema huyu kijana akifanya mchezo hiyo hela itaisha na atabaki na ka biashara kadogo tuu ya kumpa hela ya kula na kuendesha maisha ila akitaka kuwa bilionea atafute washauri awalipe, na hata kusimamia investment zake,
Sasa hivi ni muajiriwa wa times...haya maisha haya wakati alikuwa na uwezo wa kufungua radio station yake
Kuna apartments flani pale roundabout ya kuelekea Giraffe hotel niliona kaweka katika mitandao kwamba kanunua kamoja..kuna jamaa yangu anahudumia zile nyumba taarifa alizokuja kunipa nilichoka kabisa na nikamuona huyu Idrissa ni mngese kweli
Hahaha...sawa mkuu hakuna shida nakuelewa sana hiyo ilikua "poking"Sijadili habari za kimbeya humu.. Huu uzi ungeandikwa Idris sijui ameachana na Wema au anadate na fulani wala usingeona comment yangu..
Kijana mdogo kuchezea Million 500 ndani ya miaka miwili ikapotea hii habari hata Prof Ngowi wa pale Mzumbe ukienda kumwambia ataijadili.. Hata baba yako ukikaa nae sebuleni ukimpa habari kama hii mtajadiliana..
Si ndio hao kasema wameharibu hela zake?! Washauri wenyewe hapa bongo wapigaji, wanaangalia wakupige vipi!
Nilivyosikia kanunua nyumba na bmw nikajiuliza sasa amebaki na sh ngapi?Hakwenda kwa washauri aache uongo... Yaani wale waliokufanyia kampeni ushinde BBA hawana ujuzi wowote ndio wawe washauri wa mambo ya biashara?? Si angemtafuta hata huyu chige akamsaidia?? Mshauri anakuruhusu ununue nyumba na BMW kabla hata ya kutupa kiasi kwenye Investment ambayo return yake itaonekana, mshauri anakwambia ufanye biashara ya T-shirts sijui video games..
Nilivyosikia kanunua nyumba na bmw nikajiuliza sasa amebaki na sh ngapi?