Idris Sultan Yamemfika Hapaa

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
643
Reaction score
845
Msanii wa kuchekesha Idris Sultan amejitoa Rasmi katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kinachosemekana kuwa ni maji kumfika shingoni. Watu wa karibu wa Idris wanasema kuwa Mchekeshaji huyo maarufu Tz amekerwa na tabia ya mashabiki wake kumuita Shemeji wakati yeye Kula hali. Mmmmmh..!

Amesema kwamba yeye ana jina lake na kama angejua kama haya yote yatatokea leo basi asingekubali toka mwanzo kuitwa shemeji, amekasirishwa sana na matusi anayotukanwa pindi akiwaposti wanawake wengine hata dada zake. Pia wapo waliodai kuwa anatafuta kiki na anamuiga Justine Beiber kwasababu siku sio nyingi ataifungua tena na kuendelea na vichekesho vyake kama kawa.

Haya sasa Wenye shemeji mpo.? #mckonjetv
 
Tatizo anapenda kuyaleta mambo ya chumbani hadharani na ndicho kinachomcost. Ukikosana na Wema, halafu ukaamua kujifanya kuziweka hisia zako au ugomvi wako na wema hadharani inabidi ujipange sana kupokea mashambulizi ya mashabiki wake. Nadhani hilo Idris hakulifikiria.
 
Kuna vitu vingine vinauma sana. Na hata angeyaficha bado angetafutiwa tu sababu ya kumtukana,mashabiki wa wema ni machizi hawajui kumwachia mtu privacy yake. Kumbuka hata dai alitemaga upupu hivyohivyo ig baada ya kuvumilia sana kama utakumbuka ile hashtag ya bringbackourwema,wakitaka ampe mtaji wema ajitegemee sijui nini na nini wasijue kinachoendelea nyuma ya pazia jamaa yakamfika hapaaaaaa akayamwaga hadharani
 
Wema ni Mama Mlezi wa Bongo Movies na Watoto wa Bongo Fleva, kujenga nae uhasama wowote, popote nikutafuta kupotea mazima...
Kaka Simba kaona nyota inafifia ameanza kutafuta ushoga kwa Godmother!
 
Juzi alikataa kwenda Escape One anadai yeye si shemeji.
Usidanganye,hakwenda kozi wema hajawahi kwenda kumpa sapoti kwenye events zao za fun fellas. Na alitoa maelezo why hakutaka kuitwa shemeji.

All in all hawa watu walikuwa wanaigiza kuanzia kwenye preg na mambo yao kiukweli kwa mtu makini utajua tu kuwa zilikuwa ni drama na kama kulikuwa na rshp basi iliishaga muda sema ndo hvy jamaa alikuwa akikifikiria kichambo cha team wema. Tuendako wanaume watamwogopa wema sababu ya team yake
 

Kwa kweli, hata mimi nimemuelewa sana Idris. Relationship yake na Wema imekua ni yake na the rest of team Wema. Yaani wakikosana na Wema kidogo tuu akina Dougiemasta wanaanza kumtukana instagram. Sasa kaka wa watu amechoka. Hap team Wema wanamuharibia sana Wema, hivi hivi walimsakama Diamond na ile "bring back our wema" haya yameishia wapi? Idris kama ana akili asepe, maana wameshaanza kusema kama sio Wema Idris asingekua na jina Tz.
 
Wema ni Mama Mlezi wa Bongo Movies na Watoto wa Bongo Fleva, kujenga nae uhasama wowote, popote nikutafuta kupotea mazima...
Kaka Simba kaona nyota inafifia ameanza kutafuta ushoga kwa Godmother!

Poleni sana. Diamond has never needed Wema wala mashabiki wa Wema. Zile campaign za team Wema za kuto kumpigia kura Diamond na kumpigia Davido last year viliishia wapi? Diamond will remain Diamond and on top of his game, and Wema's fans will remain delusional souls.
 
Ndo nawashangaa hivi Wema yy ni miss Afrika? Idriss ni mshindi wa big brother Africa na sio team wema waliomfanya awe mshindi kwn kipindi yuko bba hakuwa na mahusiano na wema. Team wema wanahitaji kibadilika na watambue nani analeta mambo yake public kama sio wema yy mwenyewe,kina dougie ambao ni marafiki zake wanapata wapi nguvu ya kumtukana idd kama sio yy mwenyewe kuwaambia ya sirini? Yaan watz tufikie kipindi tuache kuingilia mahusiano ya mastaa wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…