IEBC: Spoiled votes during digital streaming Vs Manual streaming.

zinj

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2013
Posts
1,004
Reaction score
573
Wakuu heshima kwenu,wakati tukishuhudia matokeo ya kinyang'anyiro cha Urais, kura zilizoharibika zilikuwa ni zaidi ya laki mbili (200,000) na vituo vilivyo wasilisha matokeo havikuzidi mia hamsini (150)sasa hivi wanatumia manual counting na na kura zilizo haribika ni chini ya laki mbili na vituo vilivyowasilisha matokeo ni zaidi ya awali,kulikoni?!!
 

Mkuu kama nakumbuka vizuri, jana Barozi wa Uingereza alisema kwamba idadi ya kura zilizo haribika zitapaswa kujumuishwa na zile za halali ili wapate kura zote zilizopigwa, alafu wafanye mahesabu ya kupata average kuona ni nani amepata zaidi ya asilimia 50.1% - kati ya wagombea wote wa URAIS sio Uhuru na Raila tu.

Naona tamko hilo liliwashtua IEBC ukizingatia kwamba digital streaming 4 some strange reason ilikuwa inafyatua idadi kubwa ya kura zilizo haribika!! Sina shaka kama wange endelea kutumia njia ya digitali mpaka mwisho, idadi ya kura zilizo haribika ingeweza kabisa kukaribia 900+ hivyo kumkosesha mmoja wao kura za ushindi.

Sasa baada ya kushtukia tamko/pendekezo la Barozi wa Uingereza ndio wakasema system ya dijitali imeharibika kabisa itabidi warudi back to stone age system yaani watumie njia ya manual! Nini kilitokea baada ya kutumia mfumo huo mbadala? ghafla idadi ya kura zilizo haribika ikashuka kwa kasi na hii si kwa bahati mbaya, walijua hata zijijumuhishwa kwenye hesabu za mwisho hazitabadilisha kitu kwa kuwa idadi ya kura zitakazo haribika itakuwa ni ndogo mno kiasi cha kutoweza kuathili mtu wanae mtaka - hivyo kufanya kelele za Mwingereza huyo na wenzake kuzimwa kiufundi. Jamaa hawa wa IEBC walikuwa wamejizatiti vilivyo kwa lolote, tusubiri matangazo ya mwisho ya IEBC ya nani ameshinda kinyanganyiro cha URAISI, je ushindi huo utapokewaje na msindani wao - hilo lilikuwa ni angalizo langu, nawatakieni kila kheri watu wa Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…