Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Erastus Ethekon, amesema tume haiwezi kuendesha uchaguzi katika mazingira yaliyojaa chuki, uchochezi, mgawanyiko na vurugu, huku akitoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wananchi kulinda amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati ya ngazi ya juu inayowaleta pamoja IEBC, NCIC, DCI na taasisi nyingine ili kukabiliana na matamshi ya chuki, uchochezi wa kikabila na vurugu zinazohusiana na uchaguzi, Ethekon alisema mazingira salama ni msingi wa uchaguzi huru na wa haki. Alisisitiza kuwa kauli yake haikumaanisha kuwa uchaguzi umeahirishwa, bali ilikuwa onyo kuhusu umuhimu wa kudumisha utulivu kabla na wakati wa uchaguzi.
Kauli hiyo imezua mjadala mtandaoni, huku baadhi ya Wakenya wakiitafsiri kama ishara kwamba uchaguzi wa 2027 unaweza kuahirishwa. Hata hivyo, Ethekon alisisitiza kuwa ujumbe wake ulikuwa wito wa kukomesha siasa za uchochezi na kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira yanayozingatia Katiba, sheria na usalama wa wapiga kura.
Iwapo uchaguzi unategemea mazingira ya amani, nani anapaswa kuwajibika ikiwa joto la kisiasa litaongezeka hadi kuhatarisha mchakato wa kidemokrasia?