IEBC yamuita Hassan Omar - Kauli yake ya waliokufa watapiga Kura 2027 yamponza

IEBC yamuita Hassan Omar - Kauli yake ya waliokufa watapiga Kura 2027 yamponza

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
1528.jpg
1529.jpg
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imemtaka Katibu Mkuu wa Chama Tawala UDA, Hassan Omar kufika mbele yake, kujibu kauli alizotoa katika mkutano wa kisiasa Mombasa kuhusu uwezekano wa kutumia alama za vidole za watu waliofariki kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2027.


Katika taarifa ya Jumatano, Oktoba 14, 2026, IEBC ilisema Omar anatarajiwa kufika mbele ya Kamati ya Utekelezaji wa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi mnamo Oktoba 21, 2026, katika Majengo ya Anniversary Towers, Nairobi.
1527.jpg


Kauli inayozungumziwa ilitolewa wakati wa mkutano wa kisiasa Mombasa mnamo Septemba 11, 2026. Omar alizungumzia kuchukua alama za vidole za mtu aliyefariki kabla ya kuzikwa na kuzitumia katika mfumo wa BVR kupiga kura kwa ajili ya ushindi wa Rais William Ruto. Matamshi hayo yalizua mjadala kuhusu uadilifu wa uchaguzi ujao na uwezo wa mifumo ya uchaguzi kuzuia udanganyifu. Baadaye, Omar alieleza kuwa kauli zake zilikuwa zimeondolewa kwenye muktadha, akisema nia yake ilikuwa kusisitiza umuhimu wa kila raia kushiriki katika uchaguzi.

Serikali pia ilijitenga na matamshi hayo kupitia Msemaji wa Serikali, Charles Owino, akisema yalikuwa maoni ya Omar binafsi na akaitaka IEBC kuchukua hatua stahiki dhidi yake.

Sasa IEBC imesema Omar atapewa nafasi ya kujibu madai hayo kabla ya kamati kufanya uamuzi.

Soma Pia: Hassan Omar: Hata waliokufa watakuwa na alama za vidole na watapiga kura

Je, ikiwa kiongozi wa Chama Tawala anatoa kauli kuhusu kutumia alama za vidole za marehemu kupiga kura, IEBC inapaswa kufanya nini ili kuhakikisha Wakenya wanaamini uchaguzi ujao utakuwa huru na wa haki?
 
View attachment 3690609View attachment 3690610Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imemtaka Katibu Mkuu wa Chama Tawala UDA, Hassan Omar kufika mbele yake, kujibu kauli alizotoa katika mkutano wa kisiasa Mombasa kuhusu uwezekano wa kutumia alama za vidole za watu waliofariki kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2027.
View attachment 3690611

Katika taarifa ya Jumatano, Oktoba 14, 2026, IEBC ilisema Omar anatarajiwa kufika mbele ya Kamati ya Utekelezaji wa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi mnamo Oktoba 21, 2026, katika Majengo ya Anniversary Towers, Nairobi. View attachment 3690612

Kauli inayozungumziwa ilitolewa wakati wa mkutano wa kisiasa Mombasa mnamo Septemba 11, 2026. Omar alizungumzia kuchukua alama za vidole za mtu aliyefariki kabla ya kuzikwa na kuzitumia katika mfumo wa BVR kupiga kura kwa ajili ya ushindi wa Rais William Ruto. Matamshi hayo yalizua mjadala kuhusu uadilifu wa uchaguzi ujao na uwezo wa mifumo ya uchaguzi kuzuia udanganyifu. Baadaye, Omar alieleza kuwa kauli zake zilikuwa zimeondolewa kwenye muktadha, akisema nia yake ilikuwa kusisitiza umuhimu wa kila raia kushiriki katika uchaguzi.

Serikali pia ilijitenga na matamshi hayo kupitia Msemaji wa Serikali, Charles Owino, akisema yalikuwa maoni ya Omar binafsi na akaitaka IEBC kuchukua hatua stahiki dhidi yake.

Sasa IEBC imesema Omar atapewa nafasi ya kujibu madai hayo kabla ya kamati kufanya uamuzi.

Soma Pia: Hassan Omar: Hata waliokufa watakuwa na alama za vidole na watapiga kura

Je, ikiwa kiongozi wa Chama Tawala anatoa kauli kuhusu kutumia alama za vidole za marehemu kupiga kura, IEBC inapaswa kufanya nini ili kuhakikisha Wakenya wanaamini uchaguzi ujao utakuwa huru na wa haki?
Kwa maoni yangu,
nadhani UDA inafaa kumtafuta SG mwingine, kwasabau Hassan Omar amekua akiibua sintofahamu nyingi sana kwenye siasa za Kenya kwa kauli zake tata, kuelekea uchaguzi mkuu 2027; ingawa pia hiyo inaweza kua ni mbinu ya kisiasa ya kupumbaza wanasiasa wamgeukie na wamshambulie zaidi Omari, na kusaha kupiga darumini kwenye mambo mengine muhimu zaidi ya wakenya.

Akiendelea kuhudumu kama SG wa UDA hadi uchaguzi mkuu 2027, bas Hassan Omar atakua miongoni mwa wanasiasa nguli na shupavu zaidi na aliepitia misukosuko mingi sana ya kisiasa Kenya. :1Head:
 
Back
Top Bottom